http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/
Articles by "ver"

Wasichana 21 waliotekwa na kundi la Boko Haram miaka miwili iliyopita, ambao waliachiliwa huru jana, wamekutana na makamu wa rais wa Nigeria Yemi Osinbajo.
Bw Osinbajo amesema wasichana wote wamo buheri wa afya. Rais Muhammadu Buhari yumo kwenye ziara rasmi nchini Ujerumani.
Afisa wa usalama ameambia BBC kwamba wasichana hao waliachiliwa huru karibu na mpaka wa Nigeria na Cameroon.
Amesema waliachiliwa kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana, ambapo wafungwa wanne wa kundi la Boko Haram waliachiliwa huru na serikali.
Lakini serikali imekanusha madai hayo kwamba makamanda wane wa Boko Haram waliachiliwa huru ndipo kundi hilo likubali kuwaachilia huru wasichana hao.
Kundi hilo liliwateka zaidi ya wasichana 250 kutoka kwenye shule ya Chibok Aprili mwaka 2014, kisa kilichoshutumiwa vikali na jamii ya kimataifa.
Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama ni miongoni mwa walioshiriki kampeni ya kutetea kuachiliwa huru kwa wasichana hao iliyokuwa na kitambulisha mada #BringBackOurGirls. chanzo BBC

Donald Trump, akiwa na bango mkononi lililoandikwa "wanawake pamoja na Trump", katika mkutano wa hadhara mjini Lakeland, Oktoba 12, 2016.
Gazeti la New York Times limechapishwa Alhamisi ya jana asubuhi ushahidi wa wanawake wawili ambao wanasema kuwa walishambuliwa kingono na Donald Trump. Mgombea urais wa chama cha Republican tayari ameumbuka na video ya mwaka 2005 ambapo anazungumzia mambo ya uasherati.
Watu wengi nchini Marekani wanajiuliza kwa nini Donald Trump hakusikia ushauri mwema kutoka kwa wajumbe wa chama cha Republican kwa ajili yake, wale waliomshauri kufunga ukurasa wa kauli zake za uasharati na hivyo kuomba tu radhi kwa yale yaliyotokea? Mgombea huyo aliamua kulipiza kisasi, na kutoa wito katika mjadala wa mwisho kwa makahaba wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton katika mwaka mwaka 1990.
Matokeo ya kauli ya Bw Trump yameanza kujitokea. Wanawake leo wanamshtumu mgombea urais wa chama cha Republican aliwapapasa kimapenzi pila idhni yao. Katika gazeti la New York Times, wanasema, kama Jessica Leeds, kuwa wamelazimika kuzungumza hadharani baada yakuangalia mjadala uliyofanyika hivi karibuni kati ya Donald Trump na Hillary Clinton.
Sehemu hii mpya tayari imegonga vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari nchini Marekani.
Jessica Leeds alisafiri katika ndege moja na Donald Trump huku wakikaa kwenye viti viwili vinavyokaribiana "Nilishtushwa ghafla na kujihisi vibaya kuona mikono yake ikinigusa shemu mbalimbali za mwili. Ilikuwa ni kama pweza, kama vile alikua na mikono sita. Mikono yake ilikua kila mahali. Na wakati aliingiza mkono wake chini ya sketi yangu nilijihisi vibaya sana, nikaamua kukimbia, " Jessica Leeds amesema.
Mwanamke wa pili anasema Donald Trump alimkumbatia kimapenzi mwaka 2005 bila idhini yake wakati alikua akifanya kazi kama afisa wa mapokezi katika kampuni yaTrump Tower, inayomilikiwa na Donald Trump.
Donald Trump amekanusha kesi hizi zamani na kusemani njama za kutaka kumuangusha kisiasa, ili ashindwe katika uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwezi Novemba.


Antonio Guterres, kutoka Ureno ndiye atakayeshikilia mikoba ya ukatibu mkuu wa UN Januari 1, 2017 baada ya katibu mkuu wa sasa raia wa Korea Kusini Ban Ki-moon kustaafu wadhifa huo.
Inaelezwa kuwa Kamishna huyo Mkuu wa zamani wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi, atakabialiana na mgogoro mkubwa tangu Vita Kuu vya Dunia. Gutteres ameteuliwa rasmi Alhamisi ya October 13, 2016 na nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kuongoza taasisi hiyo nyeti kwa miaka mitano, ikiwa ni baada ya kupokea baraka Alhamisi iliyopita kutoka nchi 15 wanachama wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Guterres amezitolea wito nchi zenye nguvu duniani kuachana na tofauti zao kuhusu Syria, wakati yakikaribia mazungumzo mapya ya kimataifa kuhusu mgogoro wa Syria ambao umewaua watu zaidi ya 300,000 na kusababisha maefu ya raia wa Syria kukimbilia nje ya nchi tangu mwaka 2001.

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget