http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

MESUT OZIL KUULA AERSENAL



Arsenal wanajipanga kumfanya Mesut Ozil kuwa mchezaji wao anayelipwa kuliko wote kwa kumpa mkataba mpya wenye thamani ya paundi 200,000 kwa wiki, kwa mujibu wa The Mirror.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani amebakiwa na miaka miwili kwenye mkataba wake, lakini baada ya kuonyesha uwezo mkubwa Gunners wanataka kumtia kitanzi kwa kumpa mkataba mpya.

Arsene Wenger ana imani mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid atakubali kujitia kitanzi kubaki Arsenal, baada ya kumpa mpya ulioambatana na bonasi za kutosha, mkataba utakaomwezesha kulipwa paundi 200,000 kila wiki - kiwango ambacho hakuna mchezaji wa Arsenal aliyewahi kukifikia.
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget