http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

KIFO CHA MCHEKESHAJI KINYAMBE PIGO KWA TASNIA YA FILAMU TANZANIA


Mchekeshaji aliyekuwa anakuja juu kwa kasi Mohammed Abdallah "KINYAMBE" amefariki dunia leo usiku huko nyumbani kwao Mbeya.


Mmoja wa wanandugu wa Kinyambe amethibitisha kuwa msanii huyo wa filamu ambaye pia alikuwa akijulikana kwa jina la James, amefariki baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

Mchekeshaji huyo ambaye alikuwa akishiriki katika filamu mbali mbali za ucheshi alianza kuonekana kupitia kituo cha televisheni cha Chanel TEN katika kipindi cha vituko show.

Kinyambe atakumbukwa zaidi kwa aina pekee ya uigizaji aliokuwa akiufanya kiasi cha kuweza kujikusanyia mashabiki lukuki hapa nchini.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget