Makamu wa rais wa Maldives
amekamatwa kuhusiana na jaribio la kumuua rais wa taifa hilo, waziri wa
masuala ya ndani nchini humo amesema.
Ahmed Adeeb anazuiliwa na karibuni atashtakiwa kwa uhaini, Umar Naseer amesema kupitia Twitter
Rais
Abdulla Yameen alinusurika kifo baada ya boti aliyokuwa akitumia
kusafiri hadi mji mkuu akitoka kuhiji Mecca mwezi jana kulipuliwa.
Misukosuko ya kisiasa imekuwa ikiyumbisha Maldives miaka ya hivi majuzi.
Mzozo ulizuka baada ya Yameen kushinda uchaguzi, wapinzani wakisema kulikuwa na udanganyifu.
Maafisa wakuu wa polisi walifutwa kazi kutokana na uchunguzi wa
mlipuko huo, wiki moja baada ya rais huyo kumfuta kazi waziri wake wa
ulinzi.
Polisi wamethibitisha kwamba walimkamata Bw Adeeb akiwa uwanja wa ndege baada yake kurejea kutoka safari ng’ambo.
Bw Yameen hakuumia kwenye shambulio hilo la Septemba 28, lakini mkewe, msaidizi mmoja na mlinzi walijeruhiwa.
Post a Comment