Mshambuliaji hatari wa Stand
United, Elius Maguli ana mabao manane katika Ligi Kuu Bara na ndiye
kinara wa ufungaji, Kocha wa Simba, Dylan Kerr, amesema uwezo wa
mchezaji huyo ni aibu kwao.
Kabla ya kuanza kwa msimu huu wa
ligi kuu, Simba iliamua kuachana na Maguli ambaye amefunga mabao sawa na
yale ya timu hiyo, kwa madai kuwa uwezo wake ni mdogo uwanjani.
Kerr, raia wa Uingereza, amesema
kuwa, Maguli anastahili kupongezwa kwa kile anachofanya uwanjani na
mafanikio yake ni aibu kwa Simba ambayo ilimuacha.
“Maguli
anafanya vizuri kwa kufunga mabao nane hadi sasa, ni aibu kwa Simba,”
alisema Kerr na alipoulizwa inakuwaje anasema aibu kwao wakati naye
alishiriki kwenye kumuacha, alisema: “Kusema kweli ni yeye mwenyewe
ndiye aliyetaka kuondoka Simba.”
Katika kikosi cha Simba
anayeongoza kwa ufungaji ni Hamis Kiiza aliyefunga mabao matano na
wengine waliofunga moja-moja ni Juuko Murshid, Joseph Kimwaga na
Justice Majabvi.
Post a Comment