http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/
Articles by "MAKALA"


Shisha ni uvutaji wa tumbaku uliochanganywa na ladha za matunda mbali mbali kwa kutumia hookah. Hookah ni chombo kinachohifadhi maji na huwa ina mirija kuanzia eneo lakuchoma tumbaku kupitia maji mpaka mirija yakuvutia moshi mdomoni.
Shisha ni kitendo cha burudani iliyoenea nafasi nyingi hapa Tanzania mpaka imekua kitu cha kawaida. Burudani hii siyo tabia ya waafrika ki asili bali ni tabia ya warabu. Warabu huvuta shisha kwasababu ipo ndani ya mila yao. Watu wengi Tanzania wameiga tabia hiyo bila kujua madhara yake.
Uvutaji wa shisha inamadhara mengi kuliko uvutaji wa sigara. Hii ni kwasababu ya muda na idadi ya moshi unaovutwa. Mtu anayevuta sigara huwa anavuta mililita 30 ya moshi mara ishirini. Lakini mtu anayevuta shisha kwa saa moja, huwa anavuta mililita 500 ya moshi mara 200. Kwa ujumla anayevuta sigara anavuta takriban mililita 600 ya moshi wakati anayevuta shisha anavuta mililita 100,000 ya moshi kwa ujumla. Hivyo, mvutaji wa shisha huvuta moshi wa idadi ya sigara 100.
Madhara ya shisha hutokana na madhara yanayosababishwa na tumbaku. Tumbaku husababisha saratani aina 20, ikiwemo saratani ya mapafu, mdomo, koo, figo, kongosho, ini, tumbo na kadhalika. Tumbaku inayo chemikali sumu zinazosababisha saratani. Pamoja na hilo Chemikali sumu ndani ya tumbaku husababisha tatizo la moyo, tatizo la ufizi wa meno, kupunguza nguvu za kiume na tatizo la mapafu kwa ujumla.
Watu wengi wakivuta shisha, huwa wanatumia hookah moja. Tatizo lakutumia hookah moja ni mambukizi ya magonjwa. Kwa mfano; kama mtu moja anayo tatizo la kifua kikuu au kisamayu, kwa kutumia hookah ule ule anaweza kuwaambukiza wenzie.
Wakina dada pia wanapenda kujihusisha na mambo ya shisha. Ni muhimu kwa wale waliokuwa wajawazito waelewe kwamba uvutaji wa shisha huleta madhara kwa mtoto tumboni. Watoto wanaozaliwa kwa wale wanaotumia shisha huwa wanatatizo la mapafu pamoja na uzito mdogo sana.
Tumbaku pia huwa inayo nikotini. Nikotini inasababisha mazoea kwa wavutaji sigara na shisha. Nikotini ndicho kinachofanya mwili ipate mvutio na tumbaku (addiction). Ni vizuri watu waelewe tatizo la kuzoea shisha na ugumu wakuiacha baada yakutengeneza mazoea.
Kuna fikra moja la uwongo kwamba moshi ya shisha Ikipita ndani ya maji, huwa yanatoa chemikali sumu zinazosababisha saratani na nikotini. Huo si kweli. Utafiti zinaonyesha maji hayaondoi chemikali sumu inayopatikana ndani ya tumbaku.
Mbali na wavutaji shisha, wale watu waliokuwa pamoja na wavutaji wanaathirika kwa kuvuta hiyo moshi kwa ina moja au nyingine. Hivyo, wavutaji shisha hawaharibu afya zao tu lakini pia za wengine waliopo karibu nao.
Hizi ni baadhi ya chemikali sumu zinazopatikana ndani ya tumbaku yanaosababisha saratani (Acetaldehyde, Aromatic amines, Arsenic, Benzene, Beryllium, Cadmium, Chromium, Cumene, Ethylene oxide, Formaldehyde, Nickel, Polonium-210, Polycyclic aromatic hydrocarbons, Vinyl chloride).

         

 Tanzania ni nchi ya kiafrika ambayo bado ipo katika ulimwengu wa tatu na inajitaidi kwa kadri iwezekanavyo kujikwamuwa katika Nyanja mbalimbali kama kiuchumi,kisayansi,kielimu pamoja na kisiasa, lakini pamoja na jitihada hizo zote za serikali kuakikisha inafanya maswala ya kujikwamua katika janga zima la umasikini lakini bado wapo baadhi ya watumishi wa serikali na hata wale wa sekta binafsi wanafanya kazi kwa mazoea pia hata kwa kuwakandamiza baadhi ya watumishi  wao.



 Hivi ulishawahi kuona ama kusikia katika nchi zilizoendelea kama vile marekani,Australia pamoja na nchi zote za ulimwengu wa kwanza zikilalamika kwamba kuna ubadilifu wa fedha au ufujaji wa mali za uma? ebu tutafakari  swala hili  kwa pamoja na kwa weledi wa hali ya juu.

 Hapa ngoja tuchukulie mfano ulio hai na ambao upo katika vichwa vya watanzania wengi na hata kwa dunia nzima mnamkumbuka idd amin dada? aliekuwa raisi wa Uganda

Kiongozi huyo ambae alikuwa anatumia mabavu na unyanyasaji kwa raia wake tena kwa kuwabaka watoto na wanawake kwa kipindi hicho na kupelekea nchi hiyo kuyumba kiuchumi na kuwaacha wanachi wake wakiteseka na kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao, kweli wahenga walisema “bora kumfadhili mbuzi binadamu ana mahudhi” huu msemo unamaana ya kwamba binadamu wengi sio wenye hutu.

 Viongozi wengi wa namna hiyo upelekea vita ya wenyewe kwa wenyewe  nchi kama Tanzania,Uganda,Kenya  hata Burundi,Malawi ambazo ndo nchi Zipo  kwenyw nchi zinazoendelea utakuta viongozi wao ndio wanakuwa watu wa mbele kabisa kuipeleka nchi katika janga la kuyumba kwa uchumi mateso kwa raia wake nk.

 Mambo kama haya ya nchi za kiafrika hususani Tanzania ombayo ni nchi yenye vivutio vingi sana ulimwenguni baadhi ya vigogo upelekea wananchi wao kufa kwa njaa hii utokana na ukosefu wa mahitaji muhimu ya kibinadamu na pia viongozi wao kujilimbikizia mali ilihali wananchi wafa njaa kwa ukosefu wa maarifa kwa viongozi wa namna hiyo.

 Katika nchi yetu ya Tanzania ambayo ndio kwanza inapiga hatua katika sekta ya kiuchumi lakini wengi wa watumishi wa umma wanakuwa sio waaminifu katika majukumu yao na kupelekea kutokea kwa wizi wa fedha za wananchi, mfano mzuri ni kwa baadhi ya viongozi wetu waliotafuna pesa za sakata la tegeta escrow ambao wengi wamekingwa kutokana na ukubwa wa vyeo vyao na wengine kupelekea hata kujiuzulu wadhifa wao bila hata kufunguliwa mashtaka.

 Maandamano ya mara kwa mara yatokanayo na wananchi kudai haki zao huku wengine wakibeba mabango na kupelekea hata ukosefu wa amani miongoni mwa raia na kupelekea baadhi ya raia kupoteza maisha tena wasio na hatia kabisa kama watoto wadogo,wakina mama pamoja na wazee.

 Tuwe na kauli moja kwa kila raia wan chi yetu hii na tuwe na mshikamano kwa kila jambo tutakalo kulifanya ili iwe na faida kwa kizazi kilchopo na kizazi kijacho ili hata kije kuwa na maisha mema na yenye furaha miongon mwao,embu angalia nchi kama “LIBYIA” Ilivyo sasa kwani sio kama ile ya zamani.

 Hivyo basi tuwe na mikakati madhubuti na kwa kufanya maandamano hatutaleta haki na usawa katika jamii yetu inabidi sasa tuweke mabango chini na kuungana kuwa kitu kimoja na tusibaguane eti kisa  dini au ukabila wa mtu na jamii yoyote hile kitendo ambacho baba wa taifa alikipinga sana .

 Uroho wa madaraka miongoni mwa viongozi wetu wan chi yetu haswa ndio wamekuwa chanzo cha kupelekea mambo yote mabaya tuonayo nchini mwetu, wito kwa mashirika ya kiserikali na hata yale yasiyo ya kiserikali waungane kwa umoja na kupigania haki za raia wao kwa kupaza sauti ili kuweza kuwafichuwa wale wote wanaofuja mali za uma na kuwafikisha kwenye vyombo husika.

Utakuta baadhi ya wakuu wa kiofisi (boss) maofisini wanafanya vitu visivyo vya kiungwana kabisa yani na serikali inafumbia macho mswala kama hayo na kupelekea kudhalishwa kwa baadhi ya viongozi wasiokuwa na uadilifu makazini mwao.

  Nadiriki kusema hayo kwa maana ya kwamba nina ushahidi na mambo yote kwanza katika ofisi nyingi hapa nchini mwetu utakuta bosi ni mwenye jinsia ya kiume na anaekuja kuomba kazi ni jinsia ya kike basi hapo mkuu huyo wa ofisi atatumia cheo chake(nguvu) kumlaghai binti aombae kazi na kumtaka kimapenzi pindi binti akikataa basi masikini binti wa watu hapati kazi,hivi watanzania tunaelekea wapi? Ni muda wa kuonyesha mabadiliko na kuchoshwa kwetu kwa ukosefu huu wa heshima miongoni mwetu.

 Ifikie hatua kila mmoja wetu akemee udhalilishaji huu na kupaza sauti zetu kwa walengwa wa mambo kama haya,kwani kwa nchi yetu ni vijana wangapi hawana ajira wapo mitaani na vijiweni kazi kukaba na kuomba pesa kwa kila amwonae akikatiza barabarani,vijana hao sio kwamba hawana ujuzi wala vyeti vya shule laahasha bali ni baadhi ya watumishi wa serikali hawana hutu hata kidogo.

 Hivi nchi ya Tanzania inavivutio vingapi, je katika vivutio vyote hivyo nchi inapata pato kwa asilimia ngapi? Mpaka mtu adiriki kusema eti Tanzania nchi masikini hapana tunajidanganya wenyewe na hasa kwa ule msemo wa  wengi usemao “fanya kazi kama mtumwa ili uje uishi kama mfalme” kauli hii inatia moyo kwa vijana wengi ambao wamechoshwa na tabia za viongozi wetu wa taifa letu hili.

Wantanzania wenzangu kumbukeni kwa sasa tunakabiliwa na matukio mengi sana hapa mbeleni kaama kuisoma katiba inayopendekezwa na kuielewa mwisho tuipigie kura, pili kuna watoto wetu wanfanya mitiani yao ya kidato cha nne  na la msingi zaidi ambalo ndo limebeba mstakabali mzima wa maisha yetu kwa kipindi cha miaka mitano ni uchaguzi mkuu wa madiwani,wabunge na raisi niwasii tukumbuke miaka ya nyuma ili tufanye chaguo sahihi mwaka huu.                                                                                                                 
                                                                           MWANAAJI  EMMANUEL MASSAWE simu - 0712009716
MWARIRI CHARLES CHAMI 


Mji wa Vatikani ni dola-mji lenye eneo la kilomita za mraba 0,44 tu. Hivyo ni nchi ndogo kuliko zote duniani. Pande zote inazungukwa na Italia.
Idadi ya wakazi ni 791; raia ni 565 tu (mnamo Oktoba 2008).
Ni nchi ya Papa ambaye ni askofu wa Roma na mkuu wa Kanisa Katolikiduniani kote.
Jina limetokana na kilima cha Vatikani (kwa Kilatini: Mons Vaticanus) ndani ya jiji la Roma, upande wa magharibi wa mto Tiber.

Pamoja na Basilika la Mt. Petro, jengo la kanisa kubwa kuliko yote duniani, Vatikani ina makanisa mengine saba, jumba la Vatikani, ofisi za utawala wa Kanisa Katoliki, mabustani, stesheni ya treni, nyumba za kuishi, hosteli kwa ajili ya mafukara na makumbusho yenye hazina kubwa za sanaa kiasi kwamba nchi nzima inahesabiwa na UNESCO kuwa Urithi wa dunia (tangu mwaka 1984).

Mji wa Vatikani ni mabaki ya Dola la Papa lililotawala sehemu kubwa ya Italia ya Kati kwa karne nyingi hadi 1870.
Tangu 1860 baadhi ya maeneo hayo yalitwaliwa na Ufalme mpya wa Italia uliolenga kuunganisha sehemu zote zapeninsula ya Italia.
Utawala wa Papa juu ya mji na mkoa wa Roma ulilindwa na Ufaransa hadi 1870.
 Vita ya 1870 kati ya Ujerumani na Ufaransa ililazimisha Ufaransa kuondoa jeshi lake Roma, ambao hivyo ulitekwa na jeshi la Italia tarehe 20 Septemba 1870.
Wakati huo serikali ya Italia ilitaka kumuachia Papa Pius IX sehemu ya mji wa Roma kama eneo lake lakini Papa alikataa akitumaini Wakatoliki wa Italia na nchi nyingine duniani watalazimisha serikali ya Italia kumrudishia mji wote.
Kwa miaka 57 Mapapa walijifungia ndani ya jumba la Vatikani.
Mwaka 1929 serikali ya Benito Mussolini ilitafuta amani na Papa Pius XI aliyekuwa tayari kukubali mabadiliko.
Mkataba wa Laterani wa 11 Februari 1929 ukampa Papa mamlaka na madaraka ya nchi huru juu ya basilika la Mt. Petro pamoja na maeneo mengine.



Mkuu wa Dola ni Papa mwenyewe, kwa sasa Papa Fransisko (Jorge Mario Bergoglio). Nafasi yake ni kama mfalme wa kuchaguliwa asiyebanwa na katiba au masharti yoyote. Mambo ya utawala yako mkononi mwa gavana anayeteuliwa na Papa pia.
Vatikani ina uhusiano wa kibalozi na nchi 180 duniani kote kupitia Ukulu mtakatifu.

Vatikani ina jeshi dogo kabisa lakini lenye historia ndefu kabisa duniani. Ni kikosi cha Walinzi Waswisi ambacho kipo tangu mwaka 1506 na chenye wanajeshi 100 hivi. Wote ni Wakatoliki raia wa Uswisi kwa kuzaliwa.




Angelina Jolie ni mmoja wa wanaharakati maarufu wanaopinga dhuluma za kingono ikiwemo ubakaji
Viongozi wa kimataifa wanakutana jijini London kwa wiki nzima, kwa kongamano la kumaliza dhulma za kimapenzi katika mataifa yanayokabiliwa na mizozo.
Mkutano huo, wa siku nne umeandaliwa na Waziri wa masuala ya nchi za kigeni wa Uingereza, William Hague na muigizaji maarufu na mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa, Angelina Jolie.

Kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Pakistan imepata mkataba wa Adidas wakutengeneza mipira itakayotumika kwenye kombe la dunia 2014 nchini Brazil.
Fahamu “brazuca” Mpira utakaotumika kwenye mechi ya fainali utatengenezwa na Adidas wenyewe kwa vigezo na viwango vya mpira huo.
Huyu Khawaja Akhtar ni CEO wa Forward Sports Pvt, Pakistan.
29
Khawaja Akhtar alipata dili hiili baada ya waliokuwa na mkataba huu na Fifa kushindwa kukamilisha namba ya mipira iliyohitajika kwa muda waliopewa. Ilikuwa kampuni ya Mchina.


Timu ya taifa ya Tanzania ya watoto wa mitaani wakishikilia Kombe la Dunia walilonyakua Brazil



Timu ya taifa ya Tanzania kwa watoto wa mitaani imenyakua Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani, katika mashindano yaliyozishirikisha timu za mataifa mbalimbali duniani huko Rio de Janeiro, Brazil hapo jana.
Ikiwa imetinga fainali za Kombe la Dunia kwa watoto wa mitaani kwa mara ya pili mfululizo, timu hiyo ya Tanzania imeweza kutwaa Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani kama linavyojulikana Street Child World Cup hapa Rio de Janeiro.

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget