Leo Jumapili Simba na Azam FC zitashuka kusakata kandanda katika uwanja wa taifa, ni mechi muhimu kwa timu zote mbili itakayoamua mbio zao za ubingwa Ligi Kuu Bara
Mechi hii unaweza kuiita ya kufa na kupona ama fainali ya kuamua nani ataendelea kuifukuza Yanga katika kuwania ubingwa wa msimu huu 2015-16.

Huo utakuwa mchezo wa 16 kuzikutanisha timu hizo kwenye ligi tangu Azam FC ipande msimu wa 2008/2009, Azam ikishinda nne, Simba saba na kutoka sare mara nne.

Azam FC itawakosa wachezaji wengine kama kiungo Frank Domayo, Allan Wanga, Racine Diouf, Shomari Kapombe, ambao ni wagonjwa huku Nahodha Msaidizi Himid Mao ‘Ninja’, akiendelea kuitumikia kadi nyekundu aliyopata dhidi ya Mtibwa Sugar.

John Bocco; Mshambuliaji kipenzi cha kocha Stewart Hall wa Azam amekuwa kwenye kiwango cha juu. Ni mchezaji mahiri, mwenye nguvu na akili ingawa ni mwenye jazba na hasira za haraka haraka. Uwezo wake wa kupambana na mabeki na kutengeneza nafasi unaweza kuleta madhara katika safu ya ulinzi ya Simba.

Bocco anahitaji kuwekewa ulinzi mkali na mabeki wa Simba kwa sababu mshambuliaji huyu mrefu kulijia vuzri goli kila anapopata nafasi ya kuweza kufunga

Mudathir Yahya; Ni mchezaji aliyeteka imani ya kocha wa Azam FC Stewart Hall, uwezo wake umethibitika. Anabadilika kila mara kutokana na ugumu wa mechi na Simba wanayo kazi ya kufanya kumzuia kupata goli katika mechi ya leo. Katika Kumbukumbu za ushindi wa 2-0 dhidi ya Majimaji FC, mabao yote yaliwekwa kimaiani na Mudathir Yahya.

Kipre Tchetche; Yupo fiti asilimia 100 kuivaa Simba  kwenye mchezo wa Ligi Kuu. Tchetche alianza kufanya mazoezi tangu timu hiyo ilipokuwa ikijiandaa kwa mechi dhidi ya Majimaji. Simba ina sababu nyingine ya kuiogopa Azam FC kwa kurejea kwa mchezaji huyo msumbufu.

Hamis Kiiza 'Diego' amekuwa hatari sana anapokuwa kwenye eneo la hatari la timu pinzania na mshambuliaji huyo amekuwa akiwasumbua sana mabeki kwani mara wamekuwa hawamuoni na pindi anapoonekana basi anakuwa anashangilia kwenye kibendera.

Ibrahim Ajibu ameonyesha kuwa yeye ni mchezaji hatari anapokuwa kwenye lango la timu pinzani, makocha wote walioinoa Simba msimu huu Dylan Kerr na Jackson Mayanja wamekuwa na imani naye na hajawaangusha. Mchezaji huyu aliibuka kuwa mchezaji bora wa mwezi Januari. Azam FC wanayo sababu ya kuihofu Simba hali kadhalika kutokana na uwepo wa mkali huyu.

Mussa Hassan ‘Mgosi’ Hakuna asiyejua uwezo wa Mgosi, aliyewahi kuwa mfungaji bora kwenye msimu wa 2009/10 akiwa na Simba kurudi kwake kulirudisha matumaini ya mashabiki wa timu hiyo.

Bila kumsahu Brian Majwega aliyehamia Simba akitokea Azam, na Ugando aliyewahi kufanya maajabu dhidi ya Coastal Union kule Tanga.