Mbwana Samatta akivaa kitambaa cha unahodha kwa mara ya kwanza, ameiongoza timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kupata ushindi wa goli 1-0 ugenini
Mbwana Samatta amefunga goli hil kipindi cha kwanza akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Farid Musa goli ambalo limedumu hadi dakika 90 za mchezo huo.
Stars imefikisha pointi 4 baada ya kucheza michezo 3, matokeo hayo yanaifanya Stars ifikishe idadi sawa ya pointi na Nigeria ‘The Super Eagles’ lakini Stars ipo mbele ya Nigeria kwa mchezo mmoja. Nigeria itakutana na Misri kwenye mchezo wa kundi ilo siku ya Ijumaa.
Tanzania imepata ushindi wa kwanza katika Kundi G baada ya kuwafunga wenyeji, Chad 1-0 jioni hii Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya mjini hapa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Jean-Jacques Ndala Ngambo, Aliyesaidiwa Na Olivier Safari Kabene na Nabina Blaise Sebutu wote wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Stars ilipata bao hilo kipindi cha kwanza.
Bao hilo lilifungwa na Nahodha Mbwana Ally Samatta aliyemlamba chenga beki Beadoum Monde baada ya kupokea krosi ya winga Farid Mussa na kufumua shuti lililomshinda kipa Diara Gerard.
Zikicheza katika jua kali la Alasiri, timu zote zilishindwa kucheza soka ya kuvutia na kushambulia moja kwa moja kutokana na nyasi bandia zilizochoka za Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya kuchakaa.
Pamoja na kufunga, Samatta alikosa mabao mawili ya wazi, wakati Thomas Ulimwengu na Mwinyi Kazimoto nao pia walipoteza nafasi za kufunga.
Stars inaondoka kesho mchana Chad kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa marudiano Jumatatu Uwanja wa Taifa.
Post a Comment