Ranieri, 64 alikuwa meneja wa Chelsea kutoka 2000 -2004 na alikuwa kipenzi cha mashabiki katika Stamford Bridge licha ya kutoshinda taji.
Nafasi yake ilichukuliwa na Jose Mourinho mnamo 2004 lakini aliendelea kubaki kwenye mioyo ya mashabiki wa Chelsea tangu hapo. Muitaliano huyo ni mcheshi, babu mfano wa kuigwa na wengi na mmoja wa mashabiki wa Chelsea alionyesha ishara akisema: “Fanya Ranieri” na mashabiki wa Chelsea waliimba jina lake na “Leicester, Bingwa!” baada ya kipyenga cha mwisho dhidi ya Tottenham.
Chelsea kwa kuilazimisha Tottenham sare ya 2-2 wamempatia Ranieri ubingwa baada ya Eden Hazard kufunga goli la dakika za majeruhi. Kocha huyo wa zamani wa Chelsea alipaa kwenda Italia Jumatatu kumsalimu mama yake mwenye umri wa miaka 96 na atakaporejea Uingereza atapokelewa kama shujaa. Timu yake imeweka historia naye pia hali kadhalika.
Haya ndiyo aliyosema Hiddink akizungumzia simu ya Ranieri. “Baada tu ya kipyenga cha mwisho, dakika chache baada ya judo, nilipokea simu kutoka kwa Ranieri. Alitushukuru hasa kwa kile tulichofanya kipindi cha pili na nilimpongeza kwa kutwaa ubingwa.
Wamestahili, inashangaza na huenda hata ikaleta mshtuko kwa klabu iliyopambana hadi mwisho.
Post a Comment