Viongozi wa kimataifa wanakutana
jijini London kwa wiki nzima, kwa kongamano la kumaliza dhulma za
kimapenzi katika mataifa yanayokabiliwa na mizozo.
Mkutano huo, wa siku nne umeandaliwa na Waziri
wa masuala ya nchi za kigeni wa Uingereza, William Hague na muigizaji
maarufu na mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa, Angelina Jolie.Ni mwanzo wa kuidhinishwa kampeni ya miaka miwili kutoa uhamasisho kuhusu kutumiwa kwa ubakaji na unyanyasaji wa kimapenzi kama silaha wakati wa vita.
Waandalizi wa kongamano hilo wanasema wanataka huu uwe wakati ambapo ulimwengu utazinduka na kutangaza kwamba unyanyasaji wa kimapenzi sio jambo lisiloweza kuepukika wakati wa vita.
'Uwajibikaji wa kimataifa'
Lakini lengo sasa ni kuchukua hatua madhubuti, kuendeleza uchunguzi na kuripotiwa kwa visa hivyo vya unyanyasaji wa kimapenzi.
Pia katika kutoa usaidizi zaidi kwa waathiriwa na kuhakikisha kuwa usawa wa kijinsia unahimizwa katika operesheni za siku zijazo za kulinda amani.
Kiwango cha jukumu hilo ni kikubwa: katika miaka ya tisaini, vita vya Bosnia vilisababisha kuwepo takriban waathiriwa elfu hamsini wa unyanyasaji wa kimapenzi.
Takriban miongo miwili tangu vita hivyo vimalizike, ni wahalifu wapatao 60 pekee walioshtakiwa.www.skychami.com
Post a Comment