http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

IJUE HISTORIA YA HIFADHI YA MANYARA.



Hifadhi ya Ziwa Manyara ni maarufu sana nchini Tanzania kwa simba wanaopanda miti. aina hii ya simba hupatikanandani ya hifadhi hii pekee barani Afrika.

Umaarufu wa hifadhi ya Ziwa manyara unaongezeka kila siku kutokana na kukua kwa utalii wa ndani ambapo wananchi wengi kutoka katika mikoa ya kaskazini mwa Tanzania hupenda kutembelea hifadhi hii.
Hifadhi hii ipo ndani ya Bonde la Ufa ambalo kingo zake zinaongeza mandhari zaidi.


 Ziwa Manyara lililo ndani ya hifadhi ni kivutio kikubwa kwa watalii kutokana na wingi wa ndege aina ya korongo walio na mvuto mkubwa kwa kila mtu. Ndege hao huonekana kama pazia kubwa jeupe nyakati za mchana wanapokuwa ziwani kujipatia chakula na mapumziko.

Vilevile , umaarufu wa hifadhi ya Ziwa Manyara unakua kutokana na wingi wa wageni wanaotoka nje ya nchi. Idadi kubwa ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali nchini Tanzania hutembelea hifadhi hii kujionea maajabu ya dunia hasa viumbe wa porini, wanyama, mimea na ndege.

Wanyama wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na simba, nyati, tembo, nyani, chui, pundamilia na wanyama wengine wanaokula majani. hifadhi hii pia inasifika kwa wingi  wake wa ndege hasa heroe na mnandi ambao huonekana katika makundi makubwa na kufanya eneo hili la utalii kuwa na aina 400 za ndege wanaovutia.



Chemchem za maji moto ni maajabu mengine ndani ya hifadhi hii. Maji hayo yanayobubujika kutoka ardhini huonekana yakitoa moshi kama vile maji yanayochemka jikoni. Chemchem hizi za maji moto ya asili zimekuwa zikibubujika bila kukauka kwa kipindi cha mamilioni ya miaka.
Mji mdogo wa Mto-wa-Mbu ni kituo kikubwa cha biashara kinachotoa huduma kwa wageni wanaotembelea hifadhi ya Ziwa Manyara.Mji huu mdogo upo karibu na lango la hifadhi.
Hifadhi hii iko umbali wa kilometa 126 kutoka Arusha mjini ina ukubwa wa kilometa za mraba 330.
SEKTA YA MALIASILI
Mkoa una utajiri mkubwa wa madini ya Tanzanite ambayo yanathamani kubwa na hayapatikani mahali popote duniani isipokuwa Mkoani Manyara Wilaya ya Simanjiro eneo la Mirerani.  Madini mengine yanayopatikana Mkoani manyara ni pamoja na: Ruby, Green Garnet, Green Tourmaline na Rhodilite.
Kadhalika Mkoa una maeneo mazuri ya vivutio vya utalii ambavyo ni Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Ziwa Manyara ambako hupatikana aina mbalimbali za wanyamapori kama Simba, Chui, Chita, Twiga, Pundamilia, Swala, Nyati, Pofu, Ngiri, Mbuni, Korongo nk
 Zaidi ya hayo, Ziwa Manyara limepata sifa ya ziada duniani kote kutokana na kuwa ni eneo la mazalia ya ndege wengi aina ya Korongo ambao ni Kivutio cha Watalii.

Ziwa hili pamoja na Maziwa Burunge na Balangida yaliyopo Mkoani na Ziwa Natron lililopo Mkoani Arusha yalitokana na tukio kubwa  la tetemeko la Ardhi.
Maziwa mengine maarufu katika Mkoa ni Ziwa Babati, Balangdalalu, Bassotu na bwawa la Nyumba ya Mungu. Maziwa yote hutumika katika shughuli za Uvuvi na Utalii. Aidha, maji yatokanayo na bwawa la Nyumba ya Mungu hutumika kuzalisha Umeme kwa ajili ya matumizi ya Taifa zima
Vilevile, Mkoa una eneo kubwa sana (hekta  927,526) la hifadhi  za Misitu zilizohifadhiwa kisheria ambapo jumla ya hekta 71,326 zilihifadhiwa tangu mwaka 1970 kwa mfumo wa Ubia baina ya Serikali Kuu na Serikali za Vijiji 44. 
Misitu iliyohifadhiwa ni Nou uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Haraa katika Wilaya ya Babati na Hifadhi ya Mlima Hanang katika wilaya Hanang. Misitu mingine inasimamiwa na kuendelezwa na Jamii  ngazi ya Vijiji. (Community Based Forest Management).

 Hadi kufikia mwaka 2010 Jumla ya vijiji 86 vimeanzisha misitu ambayo inamilikiwa na vijiji hivyo kisheria yenye ukubwa wa hekta 856,200.
                  
                       Mtawanyiko wa misitu katika kila wilaya.

Wilaya
Hifadhi za Serikali Kuu (Ha)
Hifadhi za Vijiji (Ha)
Jumla (Ha)
Mbulu
39,856
2,092
41,948
Hanang
5,871
13,211
19,082
Babati
25,133
34,166
59,299
Kiteto
466
791,731
792,197
Simanjiro
-
15,000
15,000
Jumla
71,326
856,200
927,526
Kuanzia Mwaka 2002 hadi sasa Mkoa umepanda  jumla ya miti 30,898,259 kufuatia makubaliano ya kila Wilaya kukuza na kupanda miche 1, 500,000 kwa kila mwaka ikiwa ni njia ya kutunza na kuhifadhi Mazingira. 

Kutokana na kuwepo kwa maliasili ya misitu baadhi ya wananchi wameanzisha zaidi ya vikundi 77 Vyenye Wafugaji nyuki 4,484. Vikundi hivi vina jumla ya mizinga 99,346 inayozalisha Asali kwa Wingi.  Shughuli hizi hufanyika katika misitu ya asili na ya watu

Asili ya Hifadhi  ya Ziwa  Manyara:
Jina  la hifadhi ya Taifa  ya ziwa Manyara  limetokana na neno lililotoholewa  kutoka  katika lugha ya kabila la Wamaasai (Emanyara) lenye  kumaanisha  mmea wa asili  ujulikanao  Kiswahili kama ‘Mnyaa.
 Kisayansi  mmea  huu  unafahamika  kama (Eurphorbia tirucalii) na  katika lugha  ya  Kiingereza unafahamika kama  (Milk bush  au  Finger  Eurphorbia) na  huwa  unatoa  utomvu  mweupe  ambao  ukipenya  katika  macho  huleta  upofu.
Mimea  mingineyo ambayo  ni jamii  au kundi la EURPHORBIA ni pamoja  na mmea unaofahamika  MTOMVU (Eurphorbia Candelabram) katika  lugha ya Kiingereza.
Jamii ya Kabila la Wamaasai  hutumia mmea huu  katika kutengeneza uzio wa  maboma  yao wanayoyatumia  kama makazi. Ambapo hifadhi  hii inapatikana  katika mji  maarufu  wa Kitalii  wa mto wa mbu  katika  Mkoa wa Arusha  na hifadhi hii ya taifa ya ziwa  Manyara  inapatikana  ndani  ya Bonde la  ufa la Mashariki.

 Kuna maandalizi muhimu ya kuzingatia wakati wa kutembelea hifadhi ya ziwa manyara
Maandalizi  hayo nilazima yazingatie huduma za malazi au  kulala,  chakula, usafiri  na mengineyo mengi  yaliyo muhimu.
Kuanzishwa kwa hifadhi hiyo
Hifadhi ya Taifa ya ziwa Manyara ilianzishwa  mwaka 1960. Hifadhi hii  iliyoanzishwa  mwaka mmoja  kabla  ya uhuru wa nchi yetu  ina hadhi ya Kimataifa kutokana na umuhimu wake wa kipekee  kwa faida  ya dunia  nzima kama eneo  la  utalii inayotambuliwa  na Shirika  la umoja  wa mataifa  linaloshughulikia  Elimu, Sayansi na utamaduni (UNESCO).
Kwa kipindi hicho kulikuwa na watalii pamoja na mwandishi maarufu wa Kimarekani,mwandishi mmoja aliyejulikana  kama Ernest Hemingway pia aliweza kutembelea hifadhi hiyo na kuandika vitabu vinavyoelezea hifadhi hiyo

Hifadhi  ya Taifa  ya ziwa  Manyara  ina  ukubwa wa eneo  la Kilomita za mraba 330 (Kilomita za mraba  220  ni za eneo  la ziwa  Manyara  na Kilomita  za mraba 110 ni  nchi  kavu). 
Kadiri siku zinavyoendelea ukubwa wa eneo  la hifadhi  ya ziwa  Manyara  unabadilika   endapo pataongezwa sehemu ya msitu  wa Marang na vile vile  sehemu ya Kaskazini  Mashariki mwa ziwa Manyara. 
          Ziwa Manyara  lina  urefu  wa kilomita  40 na upana  wake  ni  kilomita  13. Na kina chake  ni kifupi na  maji yake  ni  yenye  magadi, kama jinsi  ilivyo  kwa maziwa  yote  yanayopatikana  katika upande  wa Mashariki wa bonde la  ufa.
  Ziwa  pekee  Afrika Mashariki linalopatikana katika upande huu wa mashariki  mwa bonde  la ufa  ambalo  maji  yake  si yenye  Magadi  ni ziwa  Naivasha  katika nchi ya Kenya

Hifadhi ya Taifa  ya ziwa Manyara  inafikika  kwa njia ya  usafiri wa barabara  umbali wa kilomita  130 Kusini  Magharibi  mwa  Mji wa Arusha  katika barabara  kuu ya Arusha – Dodoma. 
Ufikapo  njia panda  ya Makuyuni, Kuelekea upande  wa mkono  wako wa kulia  na kama  unatoka  uelekeo  wa Mikoa  ya  Kanda  ya Ziwa  elekea  upande  wako wa mkono  wa kushoto.
 Hata hivyo yapo maelezo yanao elekeza katika vibao maalumu.  Vile vile  hifadhi  hii ya  ziwa Manyara inafikika  umbali wa kilomita 95 kama unatokea  hifadhi  ya  Taifa  ya Tarangire. Ambapo ni mwendo  wa umbali  wa saa 2  mpaka  2.30 kutoka  Arusha  Mjini na saa 1  kutoka  hifadhi ya  Taifa  ya Tarangire.
MAUMBILE ASILIA YA KIJIOGRAFIA HIFADHINI:
Ukuta wa bonde  la  ufa  katika  upande wa  Magharibi  mwa  hifadhi  yenyewe, Ziwa Manyara  upande wa Mashariki  mwa hifadhi yenyewe, msitu wa maji  wa ardhini   ambao  chanzo chake  cha maji  yanatoka  katika msitu wa  asili  wa nyanda za juu  Kaskazini  katika Mamlaka  ya hifadhi  ya Ngorongoro.
Maji haya  husafiri chini  ardhini  takribani  mita  600 na  hatimaye  kupenyeza  katika  nyufa za kuta  za bonde la ufa  katika  hifadhi  hii  ya ziwa Manyara  na kuufanya  msitu  huu kuwa  ni  kijani kibichi wakati wote

KUNA VIVUTIO VIKUU VYA UTALII KATIKA HIFADHI HII;
Ukuta wa Bonde  la ufa katika upande wa  Magharibi  mwa hifadhi, ziwa  Manyara  upande wa Mashariki, Simba wapandao juu ya miti,  msitu wa maji  ardhini (Ground  water  forest).


Ndege wa aina  mbalimbali  pamoja na chemichemi za maji moto (Hot  water Sulphur) kusini mwa  hifadhi  hii.

WANYAMAPORI WAPATIKANAO HIFADHINI:
Viboko katika bwawa la viboko  ambayo  ni sehemu  ya mto Simba (Hippo pool),  Tembo  (ndovu),  nyati (mbogo),  simba,  Twiga, kuro, Pundamilia, Swala pala, pongo,  kima, nyani, Tumbili, ngiri,  nyumbu wa kijivu,  Digidigi (Saruya),fisi na wengineo wengi. Viumbe  hai  ndege ni pamoja  na ndege  John,  Mbuni, hondohondo wa ardhini na wengineo wengi.

Msitu  wa maji  ardhini (Ground water forest) ambapo  panapatikana  aina  mbalimbali ya mimea  ya miti kama vile  mkomba, Mlegea, Mkwaju,  migunga ya aina  mbalimbali na miti  mingineyo mingi. Uoto  wa asili  mwingineo  ni pamoja na maeneo  wazi ya uoto wa nyasi.
 Vile vile katika  upande wa magharibi  mwa hifadhi  katika  ukuta wa bonde  la ufa  kuna  uoto wa aina  mbalimbali  wa mibuyu,  migunga, mibabara au miturituri  na aina  nyinginezo za mimea  inayostahimili  kustawi  katika maeneo makame
Kwa ujumla  eneo la hifadhi  ya  taifa  ya ziwa  Manyara  inaangukia  katika eneo la uoto wa asili  wa maeneo  makame  wa Somali  - Maasai,  Na wakati mzuri wa kutembea hifadhi hii ni kipindi cha msimu wa kiangazi kuanzia mwezi Julai, Oktoba, Novemba mpaka juni.

Hifadhi ya Taifa  ya ziwa  Manyara  inapatikana karibu  kabisa  na mji  wa mto wa mbu  maarufu  kwa shughuli  za Kiutalii ambapo  huduma  kama  vile  za vyakula,  malazi na burudani zinapatikana  kwa urahisi na kwa bei  nzuri. Lakini  hata  hivyo  watanzania wazalendo  watalii wa ndani  wanaweza kujibebea  vyakula  vyao  wenyewe vya kujipikia.

Nyumba za kulala  wageni  na maeneo ya kupigia  kambi za watu  binafsi  zinapatikana  katika  Mji wa mto wa mbu,  uliopo  jirani  na karibu  kabisa  na hifadhi  yenyewe,na  kwa watanzania pamoja na watalii wa ndani  hakuna  ulazima  sana  wa kubeba  mahema ya kupigia  kambi.

Maandalizi ya usafiri,  huduma za chakula,  malazi au kulala na mengineyo ni ya muhimu  kutekelezwa  ili  kupata  hali  halisi ya  safari  yenu  ya matembezi  hifadhini,  lakini vilevile  pasipo kusahau gharama za usafiri wenyewe  uwe  wa kukodi  au wa kwenu  wenyewe.
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget