Shisha ni uvutaji wa tumbaku uliochanganywa na ladha za matunda mbali mbali kwa kutumia hookah. Hookah ni chombo kinachohifadhi maji na huwa ina mirija kuanzia eneo lakuchoma tumbaku kupitia maji mpaka mirija yakuvutia moshi mdomoni.
Shisha ni kitendo cha burudani iliyoenea nafasi nyingi hapa Tanzania mpaka imekua kitu cha kawaida. Burudani hii siyo tabia ya waafrika ki asili bali ni tabia ya warabu. Warabu huvuta shisha kwasababu ipo ndani ya mila yao. Watu wengi Tanzania wameiga tabia hiyo bila kujua madhara yake.
Uvutaji wa shisha inamadhara mengi kuliko uvutaji wa sigara. Hii ni kwasababu ya muda na idadi ya moshi unaovutwa. Mtu anayevuta sigara huwa anavuta mililita 30 ya moshi mara ishirini. Lakini mtu anayevuta shisha kwa saa moja, huwa anavuta mililita 500 ya moshi mara 200. Kwa ujumla anayevuta sigara anavuta takriban mililita 600 ya moshi wakati anayevuta shisha anavuta mililita 100,000 ya moshi kwa ujumla. Hivyo, mvutaji wa shisha huvuta moshi wa idadi ya sigara 100.
Madhara ya shisha hutokana na madhara yanayosababishwa na tumbaku. Tumbaku husababisha saratani aina 20, ikiwemo saratani ya mapafu, mdomo, koo, figo, kongosho, ini, tumbo na kadhalika. Tumbaku inayo chemikali sumu zinazosababisha saratani. Pamoja na hilo Chemikali sumu ndani ya tumbaku husababisha tatizo la moyo, tatizo la ufizi wa meno, kupunguza nguvu za kiume na tatizo la mapafu kwa ujumla.
Watu wengi wakivuta shisha, huwa wanatumia hookah moja. Tatizo lakutumia hookah moja ni mambukizi ya magonjwa. Kwa mfano; kama mtu moja anayo tatizo la kifua kikuu au kisamayu, kwa kutumia hookah ule ule anaweza kuwaambukiza wenzie.
Wakina dada pia wanapenda kujihusisha na mambo ya shisha. Ni muhimu kwa wale waliokuwa wajawazito waelewe kwamba uvutaji wa shisha huleta madhara kwa mtoto tumboni. Watoto wanaozaliwa kwa wale wanaotumia shisha huwa wanatatizo la mapafu pamoja na uzito mdogo sana.
Tumbaku pia huwa inayo nikotini. Nikotini inasababisha mazoea kwa wavutaji sigara na shisha. Nikotini ndicho kinachofanya mwili ipate mvutio na tumbaku (addiction). Ni vizuri watu waelewe tatizo la kuzoea shisha na ugumu wakuiacha baada yakutengeneza mazoea.
Kuna fikra moja la uwongo kwamba moshi ya shisha Ikipita ndani ya maji, huwa yanatoa chemikali sumu zinazosababisha saratani na nikotini. Huo si kweli. Utafiti zinaonyesha maji hayaondoi chemikali sumu inayopatikana ndani ya tumbaku.
Mbali na wavutaji shisha, wale watu waliokuwa pamoja na wavutaji wanaathirika kwa kuvuta hiyo moshi kwa ina moja au nyingine. Hivyo, wavutaji shisha hawaharibu afya zao tu lakini pia za wengine waliopo karibu nao.
Hizi ni baadhi ya chemikali sumu zinazopatikana ndani ya tumbaku yanaosababisha saratani (Acetaldehyde, Aromatic amines, Arsenic, Benzene, Beryllium, Cadmium, Chromium, Cumene, Ethylene oxide, Formaldehyde, Nickel, Polonium-210, Polycyclic aromatic hydrocarbons, Vinyl chloride).
Post a Comment