http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

VIGOGO WA NCHI NDO CHANZO CHA UMASIKINI

         

 Tanzania ni nchi ya kiafrika ambayo bado ipo katika ulimwengu wa tatu na inajitaidi kwa kadri iwezekanavyo kujikwamuwa katika Nyanja mbalimbali kama kiuchumi,kisayansi,kielimu pamoja na kisiasa, lakini pamoja na jitihada hizo zote za serikali kuakikisha inafanya maswala ya kujikwamua katika janga zima la umasikini lakini bado wapo baadhi ya watumishi wa serikali na hata wale wa sekta binafsi wanafanya kazi kwa mazoea pia hata kwa kuwakandamiza baadhi ya watumishi  wao.



 Hivi ulishawahi kuona ama kusikia katika nchi zilizoendelea kama vile marekani,Australia pamoja na nchi zote za ulimwengu wa kwanza zikilalamika kwamba kuna ubadilifu wa fedha au ufujaji wa mali za uma? ebu tutafakari  swala hili  kwa pamoja na kwa weledi wa hali ya juu.

 Hapa ngoja tuchukulie mfano ulio hai na ambao upo katika vichwa vya watanzania wengi na hata kwa dunia nzima mnamkumbuka idd amin dada? aliekuwa raisi wa Uganda

Kiongozi huyo ambae alikuwa anatumia mabavu na unyanyasaji kwa raia wake tena kwa kuwabaka watoto na wanawake kwa kipindi hicho na kupelekea nchi hiyo kuyumba kiuchumi na kuwaacha wanachi wake wakiteseka na kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao, kweli wahenga walisema “bora kumfadhili mbuzi binadamu ana mahudhi” huu msemo unamaana ya kwamba binadamu wengi sio wenye hutu.

 Viongozi wengi wa namna hiyo upelekea vita ya wenyewe kwa wenyewe  nchi kama Tanzania,Uganda,Kenya  hata Burundi,Malawi ambazo ndo nchi Zipo  kwenyw nchi zinazoendelea utakuta viongozi wao ndio wanakuwa watu wa mbele kabisa kuipeleka nchi katika janga la kuyumba kwa uchumi mateso kwa raia wake nk.

 Mambo kama haya ya nchi za kiafrika hususani Tanzania ombayo ni nchi yenye vivutio vingi sana ulimwenguni baadhi ya vigogo upelekea wananchi wao kufa kwa njaa hii utokana na ukosefu wa mahitaji muhimu ya kibinadamu na pia viongozi wao kujilimbikizia mali ilihali wananchi wafa njaa kwa ukosefu wa maarifa kwa viongozi wa namna hiyo.

 Katika nchi yetu ya Tanzania ambayo ndio kwanza inapiga hatua katika sekta ya kiuchumi lakini wengi wa watumishi wa umma wanakuwa sio waaminifu katika majukumu yao na kupelekea kutokea kwa wizi wa fedha za wananchi, mfano mzuri ni kwa baadhi ya viongozi wetu waliotafuna pesa za sakata la tegeta escrow ambao wengi wamekingwa kutokana na ukubwa wa vyeo vyao na wengine kupelekea hata kujiuzulu wadhifa wao bila hata kufunguliwa mashtaka.

 Maandamano ya mara kwa mara yatokanayo na wananchi kudai haki zao huku wengine wakibeba mabango na kupelekea hata ukosefu wa amani miongoni mwa raia na kupelekea baadhi ya raia kupoteza maisha tena wasio na hatia kabisa kama watoto wadogo,wakina mama pamoja na wazee.

 Tuwe na kauli moja kwa kila raia wan chi yetu hii na tuwe na mshikamano kwa kila jambo tutakalo kulifanya ili iwe na faida kwa kizazi kilchopo na kizazi kijacho ili hata kije kuwa na maisha mema na yenye furaha miongon mwao,embu angalia nchi kama “LIBYIA” Ilivyo sasa kwani sio kama ile ya zamani.

 Hivyo basi tuwe na mikakati madhubuti na kwa kufanya maandamano hatutaleta haki na usawa katika jamii yetu inabidi sasa tuweke mabango chini na kuungana kuwa kitu kimoja na tusibaguane eti kisa  dini au ukabila wa mtu na jamii yoyote hile kitendo ambacho baba wa taifa alikipinga sana .

 Uroho wa madaraka miongoni mwa viongozi wetu wan chi yetu haswa ndio wamekuwa chanzo cha kupelekea mambo yote mabaya tuonayo nchini mwetu, wito kwa mashirika ya kiserikali na hata yale yasiyo ya kiserikali waungane kwa umoja na kupigania haki za raia wao kwa kupaza sauti ili kuweza kuwafichuwa wale wote wanaofuja mali za uma na kuwafikisha kwenye vyombo husika.

Utakuta baadhi ya wakuu wa kiofisi (boss) maofisini wanafanya vitu visivyo vya kiungwana kabisa yani na serikali inafumbia macho mswala kama hayo na kupelekea kudhalishwa kwa baadhi ya viongozi wasiokuwa na uadilifu makazini mwao.

  Nadiriki kusema hayo kwa maana ya kwamba nina ushahidi na mambo yote kwanza katika ofisi nyingi hapa nchini mwetu utakuta bosi ni mwenye jinsia ya kiume na anaekuja kuomba kazi ni jinsia ya kike basi hapo mkuu huyo wa ofisi atatumia cheo chake(nguvu) kumlaghai binti aombae kazi na kumtaka kimapenzi pindi binti akikataa basi masikini binti wa watu hapati kazi,hivi watanzania tunaelekea wapi? Ni muda wa kuonyesha mabadiliko na kuchoshwa kwetu kwa ukosefu huu wa heshima miongoni mwetu.

 Ifikie hatua kila mmoja wetu akemee udhalilishaji huu na kupaza sauti zetu kwa walengwa wa mambo kama haya,kwani kwa nchi yetu ni vijana wangapi hawana ajira wapo mitaani na vijiweni kazi kukaba na kuomba pesa kwa kila amwonae akikatiza barabarani,vijana hao sio kwamba hawana ujuzi wala vyeti vya shule laahasha bali ni baadhi ya watumishi wa serikali hawana hutu hata kidogo.

 Hivi nchi ya Tanzania inavivutio vingapi, je katika vivutio vyote hivyo nchi inapata pato kwa asilimia ngapi? Mpaka mtu adiriki kusema eti Tanzania nchi masikini hapana tunajidanganya wenyewe na hasa kwa ule msemo wa  wengi usemao “fanya kazi kama mtumwa ili uje uishi kama mfalme” kauli hii inatia moyo kwa vijana wengi ambao wamechoshwa na tabia za viongozi wetu wa taifa letu hili.

Wantanzania wenzangu kumbukeni kwa sasa tunakabiliwa na matukio mengi sana hapa mbeleni kaama kuisoma katiba inayopendekezwa na kuielewa mwisho tuipigie kura, pili kuna watoto wetu wanfanya mitiani yao ya kidato cha nne  na la msingi zaidi ambalo ndo limebeba mstakabali mzima wa maisha yetu kwa kipindi cha miaka mitano ni uchaguzi mkuu wa madiwani,wabunge na raisi niwasii tukumbuke miaka ya nyuma ili tufanye chaguo sahihi mwaka huu.                                                                                                                 
                                                                           MWANAAJI  EMMANUEL MASSAWE simu - 0712009716
MWARIRI CHARLES CHAMI 
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget