Yafuatayo ni baadhi tu ya maradhi yatokanayo na utumiaji wa tumbako.
1.Kung’oka kwa nywele
2.Magonjwa ya macho
3.Kukunjana kwa ngozi
4.Magonjwa ya masikio
5.Saratani ya ngozi
6.Magonjwa ya meno
7.Magonjwa ya mapafu m.f. Kansa ya mapafu,TB
8.Mifupa
9.Ugonjwa wa moyo
10.Vidonda vya tumboni
11.Magonjwa ya kucha za vidole kupinda na kuoza.
12.Kuzaa mtoto mfu.
13.Kuzaa mtoto njiti(Premature)
14.Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake.
15.Upungufu wa nguvu za kiume.
16.Kuwahi kumaliza mapema tendo la ndoa(Premature ejaculation).
17.Magonjwa ya ngozi
18.Ugonjwa wa ‘Buerger’
19.Saratani ya ini,
20.Saratani ya koo.
21.Kisukari kwa mgojwa wa kisukari sukari upanda katika damu kwa sababu sigara upelekea kuzalishwa kwa haemoglobin aina ya A1C Kwa 34%.Hivyo kuidhibti inakuwa shida na kwa asiye na kisukari anakuwa hatarini kuugua kisukari.
22.Maradhi ya figo.
Haya ni baadhi tu ya maradhi na madhara yatokanayo na sigara.
PIA MVUTA SIGARA ANANUKA AKIKUPUMULIA.
Kila sekunde nane, mtu mmoja hufariki kutokana na utumizi wa tumbako. Imebainika kuwa saba kati ya wavutaji sigara kumi, huanza uraibu huu wakiwa wangali watoto. Wanaoendelea kuvuta sigara kwa muda mrefu hufupisha maisha yao kwa miaka 20 hadi 25. Sababu ni kuwa sigara ina kemikali zaidi ya 4,000 za sumu kama Nicotine,Tar,Carbon monoxide,Arsenic n.k ambazo zina uwezo wa kudhhuru afya ya binadamu. Madhara yanayosababishwa na uvutaji sigara ni mengi na yamesambaa mwilini kote.
Post a Comment