http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

SKYCHAMI

Latest Post

Philippe Coutinho sasa haiwezekani kujiunga na Barcelona akitokea Liverpool msimu huu wa majira ya joto kwa mujibu wa RAC1 kupitia Mundo Deportivo .
Madau kadhaa ya Barcelona kwa ajili ya mchezaji huyo yamekataliwa na klabu ya Liverpool imesisitiza Mbrazili huyo hauzwi.
Valencia wanakaribia kumsajili kwa mkataba wa mkopo kiungo wa Manchester United Andreas Pereira, kwa mujibu wa  Cadena Ser Valencia .
Pereira alikuwa Granada msimu uliopita na yupo mbioni kurudi kwenye La Liga msimu huu tena.
Kiungo wa Nice Jean-Michael Seri amefikia makubaliano ya mkataba wa miaka minne kujiunga na Barcelona, kwa mujibu wa  L'Equipe.
Bayern Munich wanaangalia uwezekan wa kumsajili mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Julian Draxler, kwa mujibu wa  Westdeutsche Allgemeine Zeitung .
Mustakabali wa Drazxler PSG haueleweki kufuatia usajili wa Neymar, na Mjerumani huyo amehusishwana tetesi za kutaka kutua Arsenal, Liverpool na Manchester United.
Arsenal wamempa mkataba mpya wa miaka minne Alex Oxlade-Chamberlain wenye thamani ya paundi 125,000 kwa wiki kumzuia kwenda Chelsea, kwa mujibu wa  Daily Star .
Kylian Mbappe ameachwa kwenye mazoezi ya Monaco baada ya kufanya mabishano na Andrea Raggi Jumanne iliyopita kwa mujibu wa   L'Equipe .
Arsenal wamemtoa Jack Wilshere kwa AC Mila, limeripoti  Corriere dello Sport .
Wilshere amehusishwa na tetesi za kujiunga na klabu hiyo ya Serie A siku za nyuma, lakini mchezaji huyo anasita kuondoka Ligi Kuu Uingereza.
Manchester City itaendelea kumfukuzia Alexis Sanchez hadi mwisho wa dirisha la uhamisho, na wameandaa kitita cha paundi milioni 70 kwa ajili ya nyota huyo wa Arsenal, limeripoti Mirror .
Chelsea wanajipanga kutumia paundi milioni 200 kusajili wachezaji wapya watano ili kutimiza anachokitaka Antonio Conte, kwa mujibu wa Express .
Wachezaji watatu wa Southampton Virgil van Dijk, Cedric Soares na Ryan Bertrand wapo kwenye orodha ya wachezaji anaowataka Conte, kadhalika Danny Drinkwater wa Leicester City na kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain.
Nyota wa Paris Saint-Germain Julian Draxler anawaniwa na klabu za Uingereza, Man United, Arsenal na Liverpool ikiwa ataondoka Parc des Princes, kwa mujibu wa  Mirror .
Atletico Madrid imekubali kuilipa Chelsea €55 millioni kwa ajili ya kumnunua Diego Costa, kwa mujibu wa habari.
Costa kwa sasa yupo Brazili baada ya kukataa kurejea Chelsea na klabu pekee anayoitaka kujiunga nayo kwa sasa ni Atletico Madrid.
Liverpool wamekubali kufanya mkutano wa mwisho na Barcelona kuhusu uhamisho wa Philippe Coutinho, kwa mujibu wa Sport .
Klabu hiyo ya Ligi Kuu Uingereza imekataa ofa tele kwa ajili ya mchezaji huyo, ofa ya mwisho ilikuwa euro milioni 125. 
PSG wapo mbioni kutangaza usajili wa Kylian Mbappe kutoka Monaco, kwa mujibu wa habari kutoka  Mundo Deportivo .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 atakuwa mchezaji wa pili ghali zaidi katika historia, baada ya klabu hiyo ya Paris kumsajili Neymar kwa euro milioni 222.
Real Madrid inataka kumtunuku Marco Asensio mkataba mpya hadi 2023 na kuiongeza bei yake hadi euro mlioni 500, kwa mujibu wa Marca .
Barcelona wametoa ofa ya euro milioni 30 kwa ajili ya kiungo wa Nice Jean Michael Seri katika harakati zao za kutafuta wachezaji wapya, limedai Sport.
Real Madrid imekataa ofa ya euro milioni 75 kwa ajili ya Mateo Kovacic kutoka Juventus, kwa mujibu wa AS .
West Brom wanafikiria kumsajli beki wa Liverpool Mamadou Sakho baada ya Manchester City kuonesha nia ya kumsajili Jonny Evans, kwa mujibu wa BBC .
Sakho anakadiriwa kuwa na thamani ya £30 millioni na Liverpool na aling'ara alipokuwa akitumika kwa mkopo Crystal Palace msimu uliopita baada ya kukataa kujiunga na West Brom.
Real Madrid wanajipanga kutoa dau la paundi milioni 46 kwa ajili ya kipa nambari moja wa Manchester United, David De Gea kwa mujibu wa  The Sun .
Inter imefanya jaribio la kumsajili beki wa Arsenal Shkodran Mustafi kwa uhamisho wa mkopo, kwa mujibu wa GIanlucaDiMarzio.com .
Miamba hao wa Serie A wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi na wanaamini Mjerumani huyo atakuwa suluhisho lao baada ya kumkosa Eliaquim Mangala kutoka Manchester City.
Chelsea watalazimika kukubali fedha kichele katika ofa ya Diego Costa tofauti na ile waliyotarajia wangeipata kwa biashara ya mchezaji huyo, kwa mujibu wa  Sun .
Costa amekuwa tu kama mchezaji wa ziada Darajani, na tetesi zinamhusisha kuwa kwenye mchakato wa kurejea Atletico Madrid.
Lakini miamba hao wa Ligi ya Hispania wapo tayari kulipa paundi milioni 30 tu, ikiwa ni kudogo zaidi ya paundi milioni 50 walizotoa Chelsea kumsajili mshambuliaji huyo.
Arsenal wapo tayari kumsajili Julian Draxler, na PSG wanataka kiasi cha paundi milioni 32 kukamilisha usajili wa mchezaji huyo majira ya joto, kwa mujibu wa The Times . 

Wanaume wanne wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.
Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu.
Kisha polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilipatikana.
Wanaume wanne, wawili kati yao madaktari wa kitamaduni walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua.
Walifikishwa katika mahakama ya Estcourt kilomita 175 kaskazini magharibi mwa mji wa Durban.
Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa kuna uwezekano kuwa wanaume hao wanne walio na umri wa kati ya miaka 22 na 32 ni sehemu ya genge kubwa.
Uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa zao wametowewa kujitokeza.
Wachunguzi wa visa vya uhalifu wameitwa kutambua sehemu hizo za binadamu, kwa kuwa haijulikana ikiwa sehemu hizo ni za mtu mmoja au watu kadhaa.
Mwezi mmoja uiopita mjini Durban, mwanamume mmoja alikamatwa akiwana na kichwa cha binadamu ambacho inanamiwa alikuwa na mpango wa kikiuza kwa daktari ya kitamadunia.
                                                                                                        Chanzo BBC Swahili

Kocha Mkuu wa Simba Joseph Omog, ametamba kwa kusema yeye na wachezaji wake wanatamani kesho iwe leo ili waweze kufanya mauaji iliyokusudia kwa mahasimu wao Yanga.
Kocha huyo amesema kuwa  wapo tayari kuwakabili Yanga na kwa maandalizi waliyofanya haoni kama wapinzani wao wanaweza kuepuka na kichapo.
“Kila mmoja kwenye kambi yetu wakiwepo wachezaji wanatamani kesho iwe leo kwani wamepania kuonyesha heshima ya Simba mpya lakini pia kujitangaza kuwa sisi ndiyo mabingwa wapya wa msimu utakao anza Jumamosi,”amesema Omog.
Pia amesema mechi  za kirafiki walizocheza Afrika Kusini, Dar es Salaam pamoja na Zanzibar zimemsaidia kujua matatizo ya yaliyokuwa yakikisumbua kikosi chake hivyo wanaingia kwenye mchezo na Yanga wakiwa wamekamilika kila idara.
Amesema tatizo la ukame wa mabao pia wamelimaliza na hilo limejionyesha kwenye mchezo wao wa mwisho waliocheza na Gulio ya Zanzibar na kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0, huo ukiwa ni ushindi mkubwa katika mechi zao zote za kirafiki walizocheza.
Mbali na kupania kuifunga Yanga, lakini lengo kubwa la Omog na mashabiki wa Simba ni kuiona timu yao inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu baada ya kulikosa taji hilo kwa misimu minne iliyopita.

Wayne Rooney amekuwa mchezaji wa pili kutimiza idadi ya mabao 200 katika Ligi Kuu Uingereza baada ya kufunga dhidi ya Man City usiku wa kuamkia leo  
Rooney mwenye umri wa miaka 31 amefunga bao hilo muhimu katika uwanja wa Manchester City kipindi cha kwanza kabla ya rahim sterling kuisawazishia man city dkika za lala salama na mchezo kuisha kwa sare ya 1-1 
Mwingereza huyo amekuwa mchezaji wa pili kufikisha mabao 200 ligi ya Uingereza, akiungana na gwiji  wa zamani wa Newcastle United Alan Shearer.
Shearer ambaye amestaafu soka, sasa anafanya uchambuzi kwenye kituo cha BBC, alitikisa nyavu mara 260 katika mechi 441, wakati Rooney amefikia idadi ya mabao 200 baada ya mechi 462 za ligi.
Mchezaji huyo wa zamani wa Newcastle kwa haraka alitupia ujumbe wa twitter akimpongeza mshambuliaji huyo wa Everton, aliandika: "It's been lonely in this @premierleague 200 club. Welcome and congratulations @WayneRooney."
Mshambuliaji huyo hadi sasa amefunga katika mechi zote mbili za ligi tangu aliporejea kwenye klabu ya utotoni mwake Everton akitokea Manchester United majira ya joto.
Rooney ameshinda mataji 12 katika kipindi cha miaka 13 alichodumu Old Trafford.



Festo mselia ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Mselia Enterprises anadaiwa alijiua kwa kujipiga risasi chini ya kidevu shambani kwake eneo la Msalato, nje kidogo ya mji wa Dodoma, baada ya polisi kumbaini akiwa amehifadhi shehena ya viroba, pombe ambazo serikali imepiga marufuku matumizi yake.
tukio hilo la kujia kwa festo lilisababisha mshtuko mkubwa kwa baba mzazi mzee John mselia hadi mkupelea umauti siku chache baada ya maziko ya mwanae.
tukio la kushangaza lilitokea siku ya maziko ya baba mzazi wa festo baada ya mvua kubwa ya barafu kunyesha wakati ibada ikiendelea katika kanisa katoliki la utukufu wa msalaba Umbwe.
"ilikua ibada inaelea mwishoni basi mvua ya kawaida ikaanza kunyesha wakati watu wanaaga mwili wa marehemu ndipo barafu zikaanza kushuka na kupekea hali ya taharki kwa watu na kuanza kutoka nje kushangaa ninikinaendelea na mvua ilinyesha kwa dakika kama 20 na kurejea katika hali ya kawaida."alieleza mmoja wa mashuhuda.

Baba mzazi wa Festo Mzee John Mselia wakati wa uhai wake


Michuano ya Uefa Uropa Ligi imepigwa jana usiku kwa michezo mbalimbali,Manchester United imeambulia Sare na Fc Rostov bao 1-1 ,Apolia Nicosia wakiwa nyumbani wamechapwa na Anderletch bao 1-0,
Fc Copen hagen imetakata kwa bao 2-1,Celta vigo imeichapa Fc Krasnodar 2-1,shakle imetoshana nguvu na Borussia Monchenglabach 1-1, KAA Gent imechapwa na KRC Genk 5-2, Lyon imeichapa As Roma 4-2 na Olympiakos imetoshana nguvu na Besktas kwa bao 1-1.

Mkuu wa wilaya ya Hanang Bi Sara Msafiri Ally akitoa elimu kwa mwana kaya baada ya kufanya ukaguzi wa kihenge chake cha kuhifadhia mahindi katika kijiji cha simbai.

Kufuatia kauli ya raisi John Pombe Magufuli kwamba serikali haina shamba imemlazimu mkuu wa wilaya ya hanang mweshimiwa SARA MSAFIRI ALLY  kufanya ziara katika kijiji cha Simbai wilayan hapo na kutembelea baadh ya kaya  na kujionea magala ya asili (vihenge)na  kujirizisha kuwepo kwa chakula cha kutosha kijijini hapo.

Huu ni mwendelezo wa ziara ya Bi Sara wa kutembelea maeneo mbalimbali ya hanang kutathimini na kukagua uwepo wa chakula kwanzia ngazi ya kaya mojamoja hadi ngazi ya wilaya, na hii ni kutokana na mabadiliko ya  tabia nchi baada ya wananchi kuandaa mashamba na kusubiria mvua mpaka sasa bila mafanikio hali ambayo imeleta wasiwasi mkubwa wa uhaba cha chakula siku za mbeleni.

Mkuu wa wilaya ya Hanang Sara Msafiri akikagua moja ya kihenge cha  kaya moja cha kuhifadhia mahindi katiaka kijiji cha simbai

Pamoja na ukaguzi huo mkuu huyo ametoa elimu katika mkutano wa adhara namna ya kutumia mifigo yao pamoja na kilimo kwa kuwataka wanachi hao katika kipindi hiki cha kiangazi wauze mifugo yao na kuhifadi fedha hizo benki mpaka pale kitakapo patikana chakula cha kutosha kwaajili ya mifugo ndipo wanunue tena ili kupataa mifugo wenye afya
Kwa upande wa kilimo mweshimiwa mkuu wa wilaya amewapa usharuri wanachi  hao kulima mazao zaidi ya moja kwa kilima mtama,miogo,viazi na maindi, vilevile ametoa ahadi ya kuwaletea wananchi hao msaada wa mbegu ya mtama.

Mwaka jana wilaya hii ilifanikiwa kuvuna chakula cha kutosha hali iliyopelekea kutokuwepo kwenye horodha ya wilaya zenye upungufu wa chakula hapa nchini, Hanang ni mwiongoni mwa maeneo yanyopata mvua  mara mbili kwa mwaka hali ambayo imekua ni tofauti mwaka huu.

wananchi wa wa kijiji cha simbai wakisikiliza kwa makini hotuba ya mkuu wa wilaya Bi Sara Msafiri.


Zlatan Ibrahimovic anaamini ameliteka soka la Uingereza ndani ya kipindi cha miezi mitatu tangu alipotua Manchester United.
Mshambulizi huyo wa United amesema hana malengo binafsi yaliyobakia kwake badala yake ameelekeza nguvu na akili zake kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza.
Ibrahimovic, 35 amekuwa na ushawishi mkubwa tangu alipotua Uingereza akitokea Paris Saint-Germain kwa uhamisho huru, magoli yake 13 ya ligi yakimwacha nyuma ya Diego Costa wa Chelsea katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu.
Lakini Ibrahimovic amesisitiza kuwa lengo lake kuu ni kuisaidia United kuendeleza mwendo wao wa ushindi wa mechi tisa katika michuano yote, ligi ikiwa kipaumbele chake kikuu.
Mshambuliaji huyo aliiambia tovuti ya United: “La! Sifukuzii mtu yeyote. Nafukuzia taji kuu – Ligi Kuu.
 “Hilo ndilo dhumuni langu. Mafanikio binafsi huja kama sehemu ya malengo makuu kwa sababu hayo ni kama bonasi kwa kila mchezaji binafsi.
“Sina malengo binafsi kwa sababu nimeshayafanya, baada ya miezi mitatu katika Uingereza. Imenichukua miezi mitatu kuiteka Uingereza.
“Ikiwa kwa pamoja tunafanya vizuri, kila mtu atafanya vizuri binafsi. Najaribu kuisaidia timu na ninajaribu kufanya kile ninachokimudu zaidi – kufunga magoli, kucheza vizuri na kutengeneza nafasi kwa ajili ya wachezaji wenzangu.
United inakabiliwa na mtihani mkubwa katika mechi yao ya Jumapili dhidi ya Liverpool, na Ibrahimovic ameweka bayana kuwa lengo lao kuu ni kupunguza pengo la pointi dhidi ya timu hiyo ya Jurgen Klopp.
 “Mwezi mmoja na nusu uliopita umejidhihirisha wenyewe, pengo lilikuwa kubwa lakini sasa hali ni nzuri,” alisema.
“Tutawapa kazi kubwa sana kwa sababu nadhani duru la pili la msimu ndilo gumu zaidi. Najua tunachokitaka.
“Tuna mabonde na milima yetu tunaposhinda na kushindwa. Hivi karibuni tumekuwa tukishinda tumekuwa timu thabiti zaidi.
 “Kocha amepata kanuni nzuri, ambayo si rahisi unapokuja kama kocha mpya kwenye timu mpya na unataka kutumia falsafa yako, na aina ya uchezaji unaoutaka.
“Nilisema hapo mwanzo – pole pole, tutaimarika na mambo yamekuwa.”


Arsene Wenger ametangaza habari njema kuwa wachezaji hao watatu muhimu wamesaini mkataba mpya huku Ozil na Sanchez wakisuasua

Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Francis Coquelin wamesaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia Arsenal, klabu hiyo imetangaza.
Wafaransa hao watatu wamekuwa watu muhimu katika kikosi cha Arsene Wenger misimu ya hivi karibuni, na Giroud akiwa kinara wa mabao wa klabu hiyo msimu uliopita na Koscielny akiwa mhimili mkuu wa beki nne.
“Tuna furaha kubwa kwamba wachezaji muhimu wa timu yetu wamesaini mkataba mpya wa muda mrefu,” alisema Wenger.
“Francis ameimarika sana kiufundi miaka kadhaa iliyopita kwa sababu anajituma kila siku.
“Olivier ana uzoefu mkubwa kwenye soka sasa na amekuwa zaidi na zaidi mchezaji kamili tangu alipojiunga nasi. Laurent ni mchezaji muhimu sana wa kikosi chetu na naamini ni miongoni mwa mabeki bora wa dunia leo hii. Kwa hiyo, kwa ujumla hizi ni habari njema kwetu.”
Habari hizi zimekuja kukiwa bado na utata juu ya mustakabali wa Mesut Ozil na Alexis Sanchez ambao wanahitaji mishahara mikubwa kufanya mkataba mpya na Washika Mtutu hao wa London.wamesaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia Arsenal, klabu hiyo imetangaza.
Wafaransa hao watatu wamekuwa watu muhimu katika kikosi cha Arsene Wenger misimu ya hivi karibuni, na Giroud akiwa kinara wa mabao wa klabu hiyo msimu uliopita na Koscielny akiwa mhimili mkuu wa beki nne.
“Tuna furaha kubwa kwamba wachezaji muhimu wa timu yetu wamesaini mkataba mpya wa muda mrefu,” alisema Wenger.
“Francis ameimarika sana kiufundi miaka kadhaa iliyopita kwa sababu anajituma kila siku.
“Olivier ana uzoefu mkubwa kwenye soka sasa na amekuwa zaidi na zaidi mchezaji kamili tangu alipojiunga nasi. Laurent ni mchezaji muhimu sana wa kikosi chetu na naamini ni miongoni mwa mabeki bora wa dunia leo hii. Kwa hiyo, kwa ujumla hizi ni habari njema kwetu.”
Habari hizi zimekuja kukiwa bado na utata juu ya mustakabali wa Mesut Ozil na Alexis Sanchez ambao wanahitaji mishahara mikubwa kufanya mkataba mpya na Washika Mtutu hao wa London.

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget