Wayne Rooney amekuwa mchezaji wa pili kutimiza idadi ya mabao 200 katika Ligi Kuu Uingereza baada ya kufunga dhidi ya Man City usiku wa kuamkia leo
Rooney mwenye umri wa miaka 31 amefunga bao hilo muhimu katika uwanja wa Manchester City kipindi cha kwanza kabla ya rahim sterling kuisawazishia man city dkika za lala salama na mchezo kuisha kwa sare ya 1-1
Mwingereza huyo amekuwa mchezaji wa pili kufikisha mabao 200 ligi ya Uingereza, akiungana na gwiji wa zamani wa Newcastle United Alan Shearer.
Shearer ambaye amestaafu soka, sasa anafanya uchambuzi kwenye kituo cha BBC, alitikisa nyavu mara 260 katika mechi 441, wakati Rooney amefikia idadi ya mabao 200 baada ya mechi 462 za ligi.
Mchezaji huyo wa zamani wa Newcastle kwa haraka alitupia ujumbe wa twitter akimpongeza mshambuliaji huyo wa Everton, aliandika: "It's been lonely in this @premierleague 200 club. Welcome and congratulations @WayneRooney."
Mshambuliaji huyo hadi sasa amefunga katika mechi zote mbili za ligi tangu aliporejea kwenye klabu ya utotoni mwake Everton akitokea Manchester United majira ya joto.
Rooney ameshinda mataji 12 katika kipindi cha miaka 13 alichodumu Old Trafford.
Post a Comment