http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

HOMA YA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA YAPAMBA MOTO, SIMBA WATAMANI MASAA YAKIMBIE

Kocha Mkuu wa Simba Joseph Omog, ametamba kwa kusema yeye na wachezaji wake wanatamani kesho iwe leo ili waweze kufanya mauaji iliyokusudia kwa mahasimu wao Yanga.
Kocha huyo amesema kuwa  wapo tayari kuwakabili Yanga na kwa maandalizi waliyofanya haoni kama wapinzani wao wanaweza kuepuka na kichapo.
“Kila mmoja kwenye kambi yetu wakiwepo wachezaji wanatamani kesho iwe leo kwani wamepania kuonyesha heshima ya Simba mpya lakini pia kujitangaza kuwa sisi ndiyo mabingwa wapya wa msimu utakao anza Jumamosi,”amesema Omog.
Pia amesema mechi  za kirafiki walizocheza Afrika Kusini, Dar es Salaam pamoja na Zanzibar zimemsaidia kujua matatizo ya yaliyokuwa yakikisumbua kikosi chake hivyo wanaingia kwenye mchezo na Yanga wakiwa wamekamilika kila idara.
Amesema tatizo la ukame wa mabao pia wamelimaliza na hilo limejionyesha kwenye mchezo wao wa mwisho waliocheza na Gulio ya Zanzibar na kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0, huo ukiwa ni ushindi mkubwa katika mechi zao zote za kirafiki walizocheza.
Mbali na kupania kuifunga Yanga, lakini lengo kubwa la Omog na mashabiki wa Simba ni kuiona timu yao inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu baada ya kulikosa taji hilo kwa misimu minne iliyopita.
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget