Mkuu wa wilaya ya Hanang Bi Sara Msafiri Ally akitoa elimu kwa mwana kaya baada ya kufanya ukaguzi wa kihenge chake cha kuhifadhia mahindi katika kijiji cha simbai. |
Kufuatia kauli ya raisi John Pombe Magufuli kwamba serikali haina shamba imemlazimu mkuu wa wilaya ya hanang mweshimiwa SARA MSAFIRI ALLY kufanya ziara katika kijiji cha Simbai wilayan hapo na kutembelea baadh ya kaya na kujionea magala ya asili (vihenge)na kujirizisha kuwepo kwa chakula cha kutosha kijijini hapo.
Huu ni mwendelezo wa ziara ya Bi Sara wa kutembelea maeneo mbalimbali ya hanang kutathimini na kukagua uwepo wa chakula kwanzia ngazi ya kaya mojamoja hadi ngazi ya wilaya, na hii ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi baada ya wananchi kuandaa mashamba na kusubiria mvua mpaka sasa bila mafanikio hali ambayo imeleta wasiwasi mkubwa wa uhaba cha chakula siku za mbeleni.
Mkuu wa wilaya ya Hanang Sara Msafiri akikagua moja ya kihenge cha kaya moja cha kuhifadhia mahindi katiaka kijiji cha simbai |
Pamoja na ukaguzi huo mkuu huyo ametoa elimu katika mkutano wa adhara namna ya kutumia mifigo yao pamoja na kilimo kwa kuwataka wanachi hao katika kipindi hiki cha kiangazi wauze mifugo yao na kuhifadi fedha hizo benki mpaka pale kitakapo patikana chakula cha kutosha kwaajili ya mifugo ndipo wanunue tena ili kupataa mifugo wenye afya
Kwa upande wa kilimo mweshimiwa mkuu wa wilaya amewapa usharuri wanachi hao kulima mazao zaidi ya moja kwa kilima mtama,miogo,viazi na maindi, vilevile ametoa ahadi ya kuwaletea wananchi hao msaada wa mbegu ya mtama.
Mwaka jana wilaya hii ilifanikiwa kuvuna chakula cha kutosha hali iliyopelekea kutokuwepo kwenye horodha ya wilaya zenye upungufu wa chakula hapa nchini, Hanang ni mwiongoni mwa maeneo yanyopata mvua mara mbili kwa mwaka hali ambayo imekua ni tofauti mwaka huu.
wananchi wa wa kijiji cha simbai wakisikiliza kwa makini hotuba ya mkuu wa wilaya Bi Sara Msafiri. |
Post a Comment