Mchezo wa mwisho wa ligi kati ya Manchester United dhidi Bournemouth umesogezwa mbele na huenda ukafanyika siku ya Jumanne.
Mchezo huo ambao ulikuwa uchezwe Jumapili uliahirishwa baada ya kushukiwa kuwepo na bomu kwenye uwanja wa Old Trafford huku kikosi cha kupambana na milipuko kikiendelea na uchunguzi.
Mchezo kati ya Manchester United vs Bournemouth ulitarajiwa kuanza majira ya 11:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, ulichelewa kuanza na baadaye mchezo huo uliahirishwa kwa ushauri kutoka kwa jeshi la polisi.
Polisi nchini Uingereza imethibitisha kuwa kitu kilichokuwa kinadhaniwa kuwa ni bomu kilichoonekana kwenye uwanja wa timu ya Manchester United wa Old Trafford hakikuwa bomu kama ilivyodhaniwa bali kilikuwa ni kifaa cha wanausalama cha mazoezi kwa ajili milipuko.
Kifaa hicho kiliachwa na walinzi wa kampuni moja ya binafsi baada ya kufanya mazoezi yaliyowahusisha mbwa wenye kunusa vifaa na vitu vya kihalifu.
Kutokana na kuonekana kwa kifaa hicho mechi kati ya Manchester United na Bournemouth iliahirishwa.
Tayari kifaa hicho kimeshaharibiwa chini ya uangalizi mkali wa timu ya kuthibiti milipuko.
Tayari maafisa wa mji wametaka uchunguzi ufanyike na kuita kitendo hicho kuwa ni cha kizembe na cha kudhalilisha.
Maelfu ya mashabiki walioondolewa katika uwanja wa Old Trafford ambapo mechi baina ya wenyeji Machester United na Bournemouth iliahirishwa na itachezwa siku ya jumanne.
Post a Comment