http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

PRISONS YAPATA KOCHA MPYA (MBWANA MAKATA)


 klabu ya Tanzania Prisons imepata kocha mpya Mbwana Makata anayechukua mikoba ya David Mwamwaja aliyetimuliwa kazi siku tatu zilizopita kutokana na mwenendo mbaya uliokuwa nayo timu hiyo.

Msemaji wa Tanzania Prisons Enock Majaaliwa amesema kuwa wameamua kumpa kazi makata kutokana na kuufahamu vema uwezo wake na wanamatumani anaweza kubadilisha mwenendo wa timu hiyo kwa kuitoa kwenye hali mbaya iliyopo kwa sasa.
“Tumemchukua Mbwana Makata kocha ambaye aliwahi tuliwahi kufanya naye kazi siku za nyuma tumeamua kumrudisha kwa sababu ya CV yake aliyokuwa nayo tukiamini atakuwa msaada mkubwa wa kuiokoa Tanzania Prisons isishuke daraja,”amesema Majaliwa.
Mtihani wa kwanza kwa Mbwana Makata utakuwa Jumapili dhidi ya Stand United pambano likipigwa kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya kabla ya kutua Prisons Makata alikuwa akiifundisha timu ya JKT Oljoro iliyokuwa ikipambana kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao lakini haikuweza kufanikiwa ikikosa pointi moja nyuma ya Toto Afrika ya Mwanza.

Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget