Azam kwa sasa wapo katika mazungumzo na makocha kadhaa akiwemo Steven Keshi na kikubwa wanachokiangalia ni ubora wa CV zao na mafanikio yao

KLABU ya Azam FC, huenda ikamnyakua kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Steven Keshi kuziba nafasi ya Joseph Omog aliyetimuliwa Jumatatu ya wiki hii baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na El Merreikh ya Sudan.
Katibu Mkuu wa Azam FC Idrissa Nassoro, amesema kwa sasa wapo katika mazungumzo na makocha kadhaa akiwemo Steven Keshi na kikubwa wanachokiangalia ni ubora wa CV zao na mafanikio waliyonayo katika timu ambazo amewahi kuzifundisha.
“Tunaendelea na kufanya mazungumzo na makocha kutoka sehemu mbalimbali dunaini lakini kuna nafasi kubwa ya Mnigeria Steven Keshi kuchukua mikoba ya Mcameroon Joseph Omog kwa sababu mazungumzo kati yetu nay eye yanaendelea vizuri na historia yake katika kufundisha soka ndiyo kitu kikubwa kinachotuvutia,”amesema Nassoro.
Keshi alikiongoza kikosi cha Nigeria kuanzia mwaka 2011 ambapo alikiongoza kutwaa ubingwa wa AFCON mwaka 2013 baada ya kushinda kwa goli 1-0 dhidi ya Burkina faso kwenye mchezo wa fainali.
Mwezi Novemba 2013 alikiongoza tena kikosi cha Nigeria kufuzu kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 baada ya kuifunga Ethiopia kwa wastani wa magoli 4-1 na kukata tiketi ya kucheza kombe la dunia lililofanyika Brazil.
Juni 2014 kikosi cha The Super Eagles kilipoteza mchezo wake dhidi ya Ufaransa kwenye kombe la dunia hatua ya 16 bora, bada ya mchezo huo Keshi alitangaza kujiuzulu kuifundisha Nigeria lakini maamuzi yake yalipingwa na shirikisho la soka la Nigeria na badala yake wakamuongezea mkataba mwingine wa kuendelea kukinoa kikoi hicho.
Octoba mwaka 2014, kikosi chake kilishindwa kushinda mechi ya mwisho ili kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) yaliyofanyika Januari mwaka huu nchini Equatorial huku Ivory Coast wakiibuka mabingwa wapya wa mashindano hayo.
Kwa sasa kikosi cha Azam kipo chini ya kocha Mganda George Nsimbe ‘Best’ lakini uongozi tayari umeshaanza kufanya harakati za kuleta kocha mwingine ambaye atasaidiana na ‘Best’ kwa ajili ya kuiimarisha Azam aliyofanya uwekezaji mkubwa katika soka la Tanzania.