http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

USHINDI WA SIMBA WA 2-0 DHIDI YA POLISI MOROWAISADIA YAPANDA HADI NAFASI YA 4

 Simba imepanda mpaka nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara kufuatia kushinda mabao 2-0 dhidi ya Polisi Morogoro.

Mabao ya Simba katika mechi hiyo iliyopigwa uwanja wa Jamhuri jioni ya leo yalifungwa na Ibrahim Hajib na Elius Maguli.
Wekundu wa Msimbazi wamefikisha pointi 20 katika nafasi ya nne baada ya kushuka dimbani mara 14.

Kagera Sugar leo wameshinda bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Bao pekee la ushindi wa Wakata Miwa limefungwa na Atupele Green katika dakika ya 30′ kipindi cha kwanza.
Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar wamefikisha pointi 21, pointi moja zaidi ya Simba walioshika nafasi ya nne.

Polisi Morogoro wameshuka mpaka nafasi ya tano wakiwa na pointi 19’ sawa na JKT Ruvu wanashuka mpaka nafasi ya 6 wakiwa na pointi 19, tofauti ipo katika mabao ya kufunga na kufungwa.
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget