http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

MESS APIGA HAT-TRICK BADO MBILI TU AMFIKIE RONALDO


wakali wa pasi katika ligi ya Hispania, La Liga, FC Barcelona wameinyuka mabao 5-0 Levante katika mechi ya ligi iliyomalizika usiku huu.
Mshambuliaji tishio duniani na mpinzani mkubwa wa mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo, Muargentina Lionel Messi amepiga mabao matatu peke yake ‘Hat-trick’.

Mbrazil, Neymar ameanza kuandika karamu ya mabao katika dakika ya 17′ na dakika ya 38′ Messi ameifungia Barca bao la pili.
Dakika ya 59′ Messi mkali wa mguu wa kushoto ameandika bao la tatu na katika dakika ya 66′ akaandika bao la nne kwa mkwaju wa penalti.
Muurguay, Luis Suarez amekamilisha karamu ya mabao baada ya kufunga bao la tano katika dakika ya 73′.
Katika mechi nyingine, Valencia imeinyuka 1-0 Getafe, wakati mechi inayoendelea sasa ni baina ya Rayo Vallecano na Villarreal.
Baadaye majira ya saa 5:00 usiku Celta Vigo watachuana na Atletico Madrid.

Pos.PlayerGoalsTeam
1Cristiano Ronaldo28Real Madrid
2Lionel Messi26FC Barcelona
3Neymar17FC Barcelona
4Carlos Bacca13Sevilla FC
5Antoine Griezmann12Atlético Madrid
5Karim Benzema12Real Madrid
7Mario Mandžukic11Atlético Madrid
8Gareth Bale10Real Madrid
8Luciano Vietto10Villarreal CF
10Sergio Garciá9RCD Espanyol
10Christian Stuani9RCD Espanyol
chanzo 
shaffih dauda
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget