http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

UHURU SULEMANI KILA TIMU ANAYOICHEZEA ANABEBEBA NDOO


Baada ya juzi mchezaji wa zamani wa Simba Sports Club, Uhuru Seleman, kufanikiwa kubeba kikombe cha ubingwa wa ligi ya daraja la kwanza akiwa na timu ya Mwadui FC kutoka Shinyanga, Mchezaji huyo anakuwa ameweka rekodi ya kutwaa mataji katika kila timu anayochezea isipokuwa timu moja tu ambayo yeye binafsi anaipenda.

Nyota huto ambaye hadi sasa tayari amezichezea timu nne za ligi kuu ya Tanzania bara pamoja na moja ya Daraja la kwanza ambayo pia imeingia rasmi ligi kuu, alipost katika mitandao wa kijamii wa Facebook akijisifia kwa kanzi nzuri anayoifanya ya kuzipatia vikombe kila timu anayocheza huku akionyesha kusikitishwa kwa kushindwa kuipa kikombe Coastal Union ambayo ndio timu anayoipenda sana.

Hii ndio rekodi ya Uhuru Seleman.
1. Mtibwa Sugar, amenyakua kikombe cha Tusker mara moja.
2. Azam FC. Kombe la Charity DR Congo mara moja, Kombe la Mapinduzi mara Moja.
3. Simba SC. Amenyakua Ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mara mbili, Kombe la Mapinduzi mara moja, Kombe la Ujirani Mwema mara moja, Kombe la Mtani Jembe mara mbili, Kombe la Ngao ya Hisani mara moja.
4. Mwadui FC.  Kombe la Ubingwa wa ligi daraja la kwanza.
Wikendi iliyopita Mwadui FC walifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi ya daraja la kwnza kwa kuifunga Africa Sports kwa bao moja mchezo ambao ulichezwa kataka uwanja wa Chamazi Jijini Dar es salaam.
chanzo shaffih dauda
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget