http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

FA WAMPUNGUZIA MATIC ADHABU CHELSEA WAJA JUU


Klabu ya Chelsea imeshangazwa na maamuzi yaliyotolewa na chama cha soka cha Uingereza FA juu ya rufaa iliyokatwa na timu hiyo kupunguza adhabu ya kiungo wake Nemanja Matic aliyoipata katika mechi ya jumamosi dhidi ya Burnley.

Kiungo huyo alipewa kadi nyekundu katika mechi hiyo waliyotoka sare ya 1-1 baada kumfanyia fujo Ashley Barnes kufuatia beki huyo kumchezea rafu mbaya na mwamuzi Martin Atkinson kushindwa kumpa kadi.
Awali kiungo huyo mserbia alifungiwa mechi 3 lakini baada ya Chelsea kukata rufaa amepunguziwa adhabu na sasa atakosa mechi mbili ila klabu hiyo haijakubaliana na maamuzi hayo ya FA.
Kwa upande mwingine wajumbe wa bodi ya mpira wa miguu ya Chelsea wamesema kuwa wamesikitishwa na maamuzi hayo yaliyotolewa na kamati ya usimamizi ya FA huku wakiamini kiungo huyo ameonewa kwa kupewa adhabu hiyo.
Hivyo Nemanja Matic ambaye amekuwa anamsaada mkubwa katika kikosi cha Jose Mourinho hasa katika upande wa ukabaji  atakosa mechi ya fainali ya kombe la capital one dhidi ya Tottenham Hotspurs pia na ile ya ligi kuu dhidi ya Westham United.
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget