mkurugenzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha Bw Joseph kagie mayagila akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya ujasiriamali chuoni hapo leo asubuhi (picha na Benson mreme) |
Mkurugenzi mkuu wa chuo cha uandishi na utangazaji
arusha ajtc bwana joseph kagie mayagila afungua rasmi
semina ya ujasiriamali kwa wanafunzi chuoni hapo.
mgeni huyo rasmi akitoa hotuba yake ya ufunguzi ameanza
kwa kutoa mongozo wa namna ya kuzifanya fedha ulizo
nazo kuongezeka cha kwanza ni kuchunga tabia yako. pia
amezitaja tabia hizo zikiwa ni pamoja na dhamira na
umuhimu wa mbegu kuwa lazima uwe na fedha ambazo
zinazalisha kipato na dhamira ya pili muda. Na ya mwisho ni
mavuno kwamba baada ya kuwa na mbegu utakuwa na
muda wa kuiotesha mbegu yako na mwisho una vuna kile
ulicho kilima.
mkurugenzi huyo akifuatilia akifuatilia kwa ukaribu mada kutoka kwa mtoa mada wa kwanza bwana Onesmo Elia mbise (picha na benson mreme) |
mtoa mada wa kwanza bwana Onesmo elia mbise akiwasilisha mada yake(picha na benson mreme) |
Awali mkuu wa kitengo cha ujasiriamali katika chuo hicho
bwana Andrea ngobole ametoa histora fupi ya semina za
ujasiriamali amesema kuwa chuo kilianza kutoa elimu ya
ujasiriamali tangu mwaka 2007.
akitangaza mafaniakio ya semina ambazo zimekuwa
zikitolewa amesema kuwa nipamoja na kufanikiwa kutoa
elimu ya ujasiriamali kwa wanafunzi zaidi ya elfu moja
(1000) na kwa sasa kuna baadhi yao wanamiliki madukuka,
saluni pamoja na kampuni.www.skychami.com
Post a Comment