http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

mashindano ya utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha A.J.T.C yaanza kutimua vumbi leo


Hatimae yale mashindano ya utangazaji  katika chuo cha uandishi wa habari na 
utangazaji arusha A.J.T.C yaanza kutimua vumbi leo

Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha  leo kimezinduwa rasmi mashindano ya utangazaji wa vipind mbalimbali vya redio  katika studio za radio chuoni hapo

Mashindano hayo ambayo yanahusisha vipindi mbalimbali vya redio vya usomji wa habari, matangazo ya vifo, vipindi maalumu na michezo yameanza kwa wakufunzi wa chuo hicho kuendesha vipindi mbalimbali.

Kipindi cha kwanza kilikuwa cha DJ Elfuraha samboto  alie endesha kipindi cha muziki mchanganyiko baada ya hapo wakaingia wasomaji wa habari madam Jackline joel pamoja na madam kagiye kikafuata kipindi cha michezo safari hii akirejea tena Elfuraha samboto

Mkuu wa idara ya utangazaji chuoni hapo bwana Onesmo elia mbise aliingia katika kipindi cha dira ya maisha, kisha kikaendelea kipindi cha matukio kilicho endeshwa na Lukas modah baada ya matukio bwana Elhuruma chao aliwaburudisha wasikilizaji kwa kipindi chake cha Gospal Time, Baada ya hapo wasikilizaji wakapata fursa ya kujuwa wasiyo yajuwa kutoka kwake madam happynes Gaudens na kipindi chake cha Usiyo yajuwa .

Baada ya utangulizi huo  wa wakufunzi kumaliza vipidi vyao ndipo lile shindano likaanza rasmi kwa darasa la mount Evarist kufunguwa dimba na kufanya vipindi vya Habari, matangazo ya vifo habari za michezo  pamoja na kipindi maalum
Mashindano hayo ambayo yanashirikisha madarasa ya  11 huku  4 yakitokea katika ngazi ya stashahada na madarasa 7 yakitokea ngazi ya
Astashahada  yanatarajiwa  kuendeshwa kwa siku  tano kuazia leo tarehe 21-27/2014 siku ya ijumaa 

Bingwa  wa mashindano hayo anatarajiwa kuibuka na kitita cha elfu 60 na kikombe chenye thamani ya shilingi laki moja  huku kila mtu binafsi atakae ingia studio kuliwakilisha darasa lake akipata zawadi.

Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget