http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

NGASA APIGA MBILI,WAKATI YANGA IKIWADOBWESHA J.T.K RUVU 4-0

DSC_0026
MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaama wamebarizi kieleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara kufuatia ushindi wa mabao 4-0 kwenye uwanja wa Taifa jioni hii dhidi ya timu iliyoanza ligi kwa kishindo, lakini kwa sasa mambo ni mdobwedo kwao, JKT Ruvu ya mkoani Pwani.
Ushindi huo muhimu inaifanya Yanga kufikikisha pointi 25, tofauti na timu mbili za Azam fc na Mbeya City zenye pointi 23 kila moja, lakini yawezekana Yanga wakaa kileleni kwa saa tu endapo timu hizo zitashinda katika michezo yao ya wikiendi hii.

Mabao ya Yanga leo hii yamefungwa na winga hatari wa klabu hiyo, Mrisho Khalfan Ngassa aliyefunga mawili ambapo katika dakika ya tatu alipiga shuti kali baada ya kufanikiwa kuwachomoka walinzi wa JKT Ruvu  na dakika ya 12 aliunganisha kama kawaida mpira wa kurusha wa beki Mbuyu Twite na kuleta shangwe kubwa kwa mashabiki waliofurika uwanjani.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zikimalizika, Yanga walikuwa nyuma kwa mabao 2-0, lakini kiukweli JKT Ruvu ndio walicheza soka zuri na la uhakika, ila Yanga waliwazidi kwa hesabu nzuri za mashambulizi ya haraka.
Kipindi cha pili kilipoanza, Yanga waliendelea kulisakama lango la JKT Ruvu na Beki Oscar Samwel Joshua aliandika bao la tatu  dakika ya pili ya kipindi cha pili akiunganisha kona  murua iliyochongwa na winga mwenye kasi kubwa,  Simon Msuva.
Kikosi cha Yanga SC:  Deo Munishi ‘Dida’, Mbuyu Twite/Ibrahim Job dk45, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Relianst Lusajo dk78, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete dk64, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza.
Kikosi cha JKT Ruvu; Sadick Mecks, Mussa Zuberi, Kessy Mapande, Omar Mtaki, Damas Makwaya/Richard Msenyi dk64, Nashon Naftali, Amos Mgisa, Haruna Adolph, Paul Ndauka, Samuel Kamutu/Abdallah Bunu dk 64 na Sosthenes Manyasi/Emmanuel Pius dk59.  
Raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo ipo katika raundi yake ya 12 inaendelea kesho (Novemba 2 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa katika miji minne tofauti.
Mgambo Shooting na Coastal Union zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Mbeya City na Ashanti United zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji wa Oljoro kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashanti United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget