STRAIKA wa AC Milan Robinho ameitwa kwenye Kikosi cha Brazil kumbadili Diego Costa kwa ajili ya Mechi zinazowakabili dhidi ya Honduras na Chile.
Brazil, ambao ndio Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia Mwakani, watacheza na Honduras hapo Novemba 16 huko Miami, USA na kisha Chile hapo Novemba 19 huko Toronto, Canada.
Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari alikuwa na nia ya kumchukua Straika wa Atletico Madrid Diego Costa ambae anang’ara huko Spain kwa kupachika Bao 13 Msimu huu lakini Mchezaji huyo ameikana Brazil kwa kusaini Barua iliyopelekwa kwa CBF, Shirikisho la Soka la Brazil, akiwaeleza nia yake kuichezea Spain.
Kugoma kwa Costa kumetoa mwanya kwa Robinho, mwenye Miaka 29, kurudi tena Kikosi cha Brazil ambako hajacheza tangu Mwaka 2011.
Lakini, Alexandre Pato, ambae alicheza Mechi 3 kati ya 4 za mwisho za Brazil, ametemwa huku Majeruhi Thiago Silva akiitwa na anaungana na Wachezaji wenzake toka Klabuni Paris Saint-Germain, Marquinhos na Maxwell, ambao wamo kundini.
Chelsea inao Wachezaji wanne kwenye Kikosi hicho ambao ni David Luiz, Ramires, Oscar na Willian.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Julio Cesar (QPR), Victor (Atletico Mineiro)
MABEKI: David Luiz (Chelsea), Dante (Bayern Munich), Thiago Silva (PSG), Marquinhos (PSG), Daniel Alves (Barcelona), Maicon (Roma), Marcelo (Real Madrid), Maxwell (PSG)
VIUNGO: Lucas Leiva (Liverpool), Hernanes (Lazio), Luiz Gustavo (Wolfsburg), Paulinho (Tottenham), Ramires (Chelsea), Oscar (Chelsea)
MAFOWADI: Jo (Atletico Mineiro), Robinho (Milan), Hulk (Zenit St. Petersburg), Bernard (Shakhtar Donetsk), Willian (Chelsea), Neymar (Barcelona).
Post a Comment