http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Dakika 810, Roma imefungwa bao moja tu!

  • Rekodi ya Roma ilikuwa matatani baada ya beki wake wa kulia, Douglas Maicon kutolewa nje kwa kadi nyekundu wakati matokeo yakiwa suluhu, lakini Bradley akafunga bao la ushindi dakika nane kabla ya pambano kumalizika baada ya kazi nzuri ya 
Daniele De Rossi   Articolo Tre
UNATAKA  kuijua timu iliyo kwenye fomu katika Ligi za Ulaya? Ni AS Roma ya Italia. Imecheza mechi tisa, imeshinda zote na imefungwa bao moja tu ndani ya dakika 810 walizocheza Ligi Kuu Italia hadi sasa.
Juzi Jumapili Roma iliendeleza makali hayo baada ya kuichapa Udinese bao 1-0 katika Uwanja wa Friuli shukrani kwa bao la dakika za majeruhi kutoka kwa kiungo wa kimataifa wa Marekani, Michael Bradley.
Rekodi ya Roma ilikuwa matatani baada ya beki wake wa kulia, Douglas
Maicon kutolewa nje kwa kadi nyekundu wakati matokeo yakiwa suluhu, lakini Bradley akafunga bao la ushindi dakika nane kabla ya pambano kumalizika baada ya kazi nzuri ya Kevin Strootman.
Roma ilicheza pambano hilo bila ya nyota wake mkongwe, Francesco Totti aliye majeruhi, pamoja na nyota wa zamani wa Arsenal, Gervinho ambaye pia ni majeruhi.
Roma imekuwa na msimu bora kwenye Serie A na kuonekana kutishia utawala wa Juventus ambayo ilitawala soka la nchi hiyo kwa zaidi ya misimu miwili mfululizo. Uhodari wa safu yake ya ulinzi ndicho kitu kinachowafanya kuwa tofauti msimu huu na kuwa timu pekee iliyofungwa mabao machache na hivyo kuwa tishio kali.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget