http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

"NILISHAWAHI KUFUNGWA JELA MIEZI 2 KWASABABU YA KUGOMBEA DEMU WA MTU".....DIAMOND PLATINUMZ

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amewahi kusota lupango ya Keko, Temeke jijini Dar es Salaam kwa miezi miwili kisa kikiwa ni kugombea demu wa mtu. Akizungumza na Amani juzi jijini Dar, Diamond alisema tukio hilo lilimtokea mwaka 2007 akiwa ‘andagraundi’ wa muziki wa kizazi kipya.
  Diamond aliyasema hayo kufuatia kuulizwa swali na paparazi wetu kwamba, amerudiana na Miss Tanzania 2006 ambaye pi ni staa wa filamu za Bongo, Wema Sepetu. Je, haogopi kufanyiwa kitu mbaya na jamaa wake ambaye ndiye anayemuweka mjini? Msikie Diamond: Mimi simwogopi mtu eti kwa sababu natembea na demu wake. Hakuna anayeweza kunifanya lolote lile, najiamini.
Mwaka wa elfu mbili na saba niligombea demu na jamaa mmoja pale Tandale (Dar). Matokeo yake jamaa akanikamata na kuniweka Gereza la Keko kwa miezi miwili, nikaachiwa baadaye, kwa hiyo sitishiki,” alisema Diamond.
 Hata hivyo, Diamond hakuweka wazi kwamba baada ya kukamatwa alipelekwa kituo gani cha polisi na mahakama gani alipandishwa kabla ya kupelekwa mahabusu ya Keko.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget