http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Rais Biya amsihi Eto'o kuichezea timu ya taifa

Samuel Eto'o

Rais wa Cameroon Paul Biya amemshawishi mwanasoka Samuel Eto'o kutafakari upya mipango yake ya kujizulu kutoka soka ya kimataifa
Mshambulizi huyo wa Chelsea alikutana na waakilishi wa Rais mjini Yaounde kujadili mustakabali wa mchezaji huyo kuhusu soka ya kimataifa.
          Baada  ya kukutana na Eto'o, alikubali kuchezea Cameroon kwa mara nyingine. Sasa atakwenda Ufaransa kujiunga na timu ya nyumbani inayojiandaa kucheza dhidi ya Tunisia katika michuano ya kufuzu kwa kombe la Dunia Brazil mwaka 2014.
Etoo mwenye umri wa miaka 32 aliambia wenzake kuwa hatacheza tena soka ya nyumbani punde tu baada ya Cameroon kuicharaza Libya na kuingia katika awamu ya pili ya kufuzu kwa kombe la dunia.
Licha ya ripoti za yeye kuacha kucheza soka, kocha wa timu ya Cameroon Volker Finke alimteua Eto'o kuchezea timu ya taifa ya Cameroon dhidi ya Tunisia ingawa mwenyewe hakuwa ametoa taarifa rasmi.
Eto'o amekuwa na uhusiano tete na maafisa wa soka nchini Cameroon katika siku za nyuma ikiwemo hata kuongoza timu ya taifa kwenye mgomo uliosambaratisha mechi ya kirafiki dhidi ya Algeria.
Eto’o aliadhibiwa kwa kupigwa marufuku kucheza mechi 15 ingawa baada ya kukata rufaa alipunguziwa adhabu hadi mechi 8
Hata baada ya adhabu yake kumalizika alikataa kuichezea Cameroon kwa miezi kadhaa.
Pia sio mara ya kwanza kwa Rais Biya kuingilia kati na kumzuia mchezaji kujiuzulu kutoka katika majukumu ya kitaifa. source bbc  posted by skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget