Maandamano ya watu waliokuwa wanaunga mkono walimu wanaodai mishahara bora zaidi nchini Brazil, yamegeuka na kuwa makabiliano kati yao na polisi katika miji ya Rio de Janeiro na Sao Paulo.
Mji wa Rio ulikuwa umesongamana watu zaidi ya 10,000 wakiandamana kwa amani Hali ya usalama nchini Brazil, ni changamoto kubwa ambayo huenda ikajitokeza zaidi wakati wa kombe la dunia mwaka 2014 na michezo ya olimpiki mwaka 2016 .
Maandamano ya hivi karibuni yalidumu kwa masaa kadhaa na yalikuwa salama mwanzoni.
Lakini usiku ulipoingia ghasia zikazuka huku waamdanamanaji wakiteketeza majengo ya serikali na wengine kuvamia benki na kuvunja mashine za pesa. Baadhi ya benki ziliteketezwa.
Waandamanaji hao pia waliiba viti kwenye benki na kuvitumia kama vizuizi kati yao na polisi.
Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozu kurejesha utulivu.Walimu wamekuwa wakidai nyongeza ya mishahara kwa miezi kadhaa sasa.
Takriban watu 50,000 walikadiriwa kuandamana ili kuwaunga mkono walimu kabla ya ghasia kuzuka lakini polisi waliweza tu kuthibitisha watu source B.B.Cposted by skychamispot.com
Post a Comment