WANASOKA 13 wameingia katika orodha ya wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Utafiti wa Mwanaspoti katika klabu zote 14 zinazoshiriki Ligi Kuu Bara umeonyesha kuwa klabu tatu; Azam, Yanga na Simba ndizo zinazolipa wachezaji wake mishahara mikubwa zaidi nchini.
Hata hivyo, Azam inaongoza kwa kuwalipa mishahara mikubwa wachezaji ikifuatiwa na Yanga na Simba.
Katika wachezaji hao 13, Azam imetoa wachezaji watano sawa na Yanga huku Simba ikitamba na wachezaji watatu kwa wachezaji wanaolipwa zaidi ya Sh 2milioni kwa mwezi.
Kundi la kwanza la wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi Tanzania ni Kipre Tchetche, Kipre Balou, Aggrey Morris, John Bocco na Brian Umony (wote Azam) na Haruna Niyonzima wa Yanga ambao kila mmoja analipwa Sh4 milioni kwa mwezi.
Kundi la pili la wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa yupo Mbuyu Twite wa Yanga, ambaye analipwa Sh3.6 milioni kila mwezi.
Kundi la tatu la wachezaji wanaotesa na mapesa kwa kulipwa mshahara mkubwa ni Abeil Dhaira na Joseph Owino wa Simba ambao kila mmoja analipwa Sh3.3 milioni kwa mwezi.
Kundi la nne linaundwa na Mrisho Ngassa wa Yanga, ambaye kila mwezi analipwa Sh2.5 milioni kutoka katika klabu ya Jangwani.
Kundi la tano la wachezaji ambao wanalipwa vizuri zaidi ni Didier Kavumbagu na Hamisi Kiiza wa Yanga pamoja na Amri Kiemba wa Simba ambao kila mmoja analipwa Sh2 milioni.
Uzuri wa mishahara ya wachezaji hao ni kwamba haikatwi kodi ya aina yoyote na ndio maana wachezaji hupokea fedha zao zote zilizoandikwa kwenye mkataba.
Uchunguzi wa Mwanaspoti, umethibitisha kuwa Azam inaongoza kwa kuwalipa mishahara mikubwa wachezaji wake na kwamba wachezaji wanaolipwa mshahara wa chini wanalipwa Sh milioni moja.
Lakini Simba na Yanga, licha ya kuwa kuna baadhi wanalipwa vizuri, bado kuna kundi la wachezaji wanaolipwa kidogo na kima cha chini kwa klabu hizo mbili ni Sh 300,000 source mwanasports.posted by skychami.blogspot.com
Post a Comment