http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

WASANII WA TANZANIA WAPATA FURSA YA KWENDA KUJIFUZA CHINA


WASANII nchini wamepewa nafasi ya kwenda China kujifunza utengenezaji wa filamu kuikuza tasnia hiyo.
Hayo yamesemwa na Mwambata wa Ubalozi wa China anayeshughulikia masuala ya utamaduni nchini, Gao Wei wakati wa hafla ya uwekaji saini makubaliano ya kuoneshwa kwa filamu ya 'Goodbye Loser' kati ya Kampuni za StarTimes na Quality Group.
"China na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri miaka na miaka. Tunafurahi kuona uhusiano huu sasa unazidi kuimarika na umeingia hadi kwenye sekta ya filamu. Filamu hii ambayo itaanza kuoneshwa nchini itasaidia wasanii wa filamu kupata elimu ya kuzalisha filamu bora zenye hadhi ya kimataifa,” alisema.
“Pia China iko tayari kutoa fursa kwa Watanzania kujifunza mbinu za kuipanua sekta ya filamu," alisema Wei.
Mkurugenzi wa Quality Group ambayo ndiyo itaonesha filamu hiyo, Utkarsh Garg alisema kuwa mahitaji makubwa ya Watanzania kwa filamu za China ndizo zimewahamasisha kuingia mkataba huo.
"Watanzania walio wengi wanapenda sana kutazama filamu halisi zinazoelezea utamaduni na maisha ya Kichina lakini wanakosa nafasi hiyo. Hilo ndilo limetuhamasisha kuja na kitu kama hiki ambapo pia itasaidia kuimarisha uhusiano wa China na Tanzania," alisema Garg.


Filamu hiyo ya 'Goodbye Loser' inaelezea historia, maisha na utamaduni wa watu wa China na hatua za kimaendeleo ambayo nchi hiyo imepiga hatua.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget