http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

GENK YA SAMATTA YATINGA 16 BORA - MAN U YAUA 4-0 HUKU ROONEY AKIJIWEKEA REKODI


Usiku wa kuamkia leo  timu ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ilicheza mchezo wake wa tano wa hatua ya Makundi ya UEFA Europa League dhidi ya timu ya Rapid Wien ya Austria.
KRC Genk katika mchezo huo wa tano walikuwa nyumbani katika uwanja wao wa Luminus, Genk wakiwa nyumbani walifanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 55 dhidi ya wageni wao Rapid Wien, kitu ambacho kimewasaidia kuibuka na ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Nikolaos Karelis dakika ya 11.
Kwa matokeo hayo Genk na Atletico Bilbao wanafuzu hatua inayofuata kutokana na wote kuwa na point 9 wakati Rapid Wien na Sassuolo ya Italia watakuwa wanasubiri mchezo wa mwisho wa kukamilisa ratiba, maana hata wakishinda watakuwa na point nane kila mmoja, point ambazo hazitoshi kuipiku Genk wala Atletico Bilbao.
kwingineko Wayne Rooney ameweka rekodi ya kufunga magoli mengi ndani ya Manchester United kwenye michuano ya Ulaya wakati wakitoa kichapo cha magoli 4-0 mbele ya Feyenoord na kuendelea kuweka matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano ya Europa League.
Nahodha huyo wa mashetani wekundu alifunga bao lake la 39 kwenye michuano ya Ulaya ndani ya klabu yake wakati akiunganisha pasi ya Zlatan Ibrahimovic  na kuwaacha wachezaji wa Feyenoord wakilaumu kuwa mfungaji alikuwa kwenye eneo la offside.
Rooney akatengeneza bao la pili ambalo lilifungwa na Juan Mata
Baadaye golikipa wa zamani wa Liverpool alijifunga wakati akiwa katika harakati za kuokoa krosi ya Ibrahimovic kabla ya Jesse Lingard kufunga biashara dakika majeruhi na kumpa Jose Mourinho ushindi mkubwa akiwa kama bosi wa United.
Sare au ushindi wa ugenini dhidi ya Zorya Luhansk kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi A siku ya Alhamisi Disemba 8, itaifanya United kufuzu hadi hatua ya 32 bora.
Kipigo hiki ndio kikubwa kwa Feyenoord kwenye Uefa Cup/Europa League. Walipoteza 5-1 dhidi ya Borussia Monchengladbach mwaka 1986.
Juan Mata amefunga mfululizo kwenye mechi za United kwa mara ya kwanza tangu Septemba 2015.
United walipiga mashuti 12 yaliyolenga goli (shots on target) dhidi ya Feyenoord, mashuti yao mengi zaidi ndani ya mchezo mmoja kwenye michuano yote msimu huu.
Feyenoord, wameshinda mechi moja tu kati ya mechi zao saba zilizopita walizocheza England kwenye michuano ya Ulaya (D2 L4).
United hawajapoteza mechi 14 za mashindano ya Ulaya kwenye uwanja wa Old Trafford (pamoja na mechi za kufuzu), wameshinda mechi zote tatu za hatua ya makundi msimu huu.
MATOKEO MENGINE

Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget