http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

BOT KUTOA MIKOPO KWENYE FURSA ZA KIJOGRAFIA ZINAZOPATIKANA TANZANIA

Gavana wa benki kuu tanzania Benno Ndulu akingumza na waandishi wa habari kuhusu fursa zinazopatikana kijografia tanzania mchana wa leo jijini Arusha (Picha na Charles Chami)

Sekta ya fedha imejipanga kulikomboa taifa kwa kutoka katika janga la umasikini kwa kutoa mikopo katika sekta mbalimbali

Akizungumza na waandishi wa habari gavana wa benki kuu Tanzania profesa Benno Ndulu amesema kuwa benki hiyo itatoa mikopo katika sekta mbalimbali huku sekta za usafiri, kilimo zikipewa kipaumbele pia kuboresha bandari zinazoizunguka nchi  ili kurahisisha huduma za bandarini

Ndulu amedai kuwa Tanzania ndo pekee iliyopo katikakati mwa nchi za kuwanzia kusini mwa Somalia mpaka Malawi. Hivyo malighafi nyingi hupitia Tanzania kwenda bara la  Asia ukilinganisha na nchi za Uganda,Burundi,Zambia,Rwanda na congo.

Mwenyekiti wa Mabenki Tanzania Charlea kimei akiwa katika mkutano na waandishi wa habari mapema hii leo jijini arusha. picha na  (Charles Chami)

Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa mabenki Tanzania Charles Kimei ameishukuru bank ya kuu na serikali kwa ushirikiano wanaopata kwa imewawezesha kuapata amana kubwa kutoka kwa wananchi pamoja na taasisi mabalimbali na kufanikiwa kiungua zaidi ya matawi mia moja mwaka huu

Kimei akizungumzia swala la mikopo amesema kuwa watatumia fursa hiyo ili waweze kutengeneza na kuimarisha miundo mbinu ya usafiri katika nchi zilizopo nje ya bahari kwa ili huduma ziweze kuwafikia walengwa.

Huu ni mkutano wa 18 wa taasisi mbalimbali za kiuchumi ulianza jana na kumalizika leo hapa jijini arusha ambapo zimejadiliwa fursa zinazopatikana kijografia hapa tanzani ambapo taasisi kama BOT,SSRA,CMSA,TIRA NA TBA Zilishiriki.

Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget