http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Nje ya pitch- SAFA waliitumia BANYANA BANYANA, TFF itumieni Kill Queens

Kabla ya ligi ya wanawake nchini Afrika Kusini, kampuni ya masuala ya petroli iitwayo Sasol walikuwa wadhamini wakuu (official sponsor) wa timu ya taifa ya wanawake wa nchi hiyo maarufu kama Banyana Banyana. Mafanikio ya Banyana Banyana yalikuwa chanzo cha chama cha soka nchini humo (SAFA) kuishawishi Sasol juu ya uwanzishwaji wa ligi kuu ya wanawake jambo ambalo lifanikiwa mwaka 2009.

Sasol walikubali kuwa mdhamini wa ligi ya juu kwa upande wa wanawake, pia benki ya ABSA ambayo ni mdhamini kwa upande wa ligi ya wanaume PSL wakaingia mkataba wa kudhamini ligi ya kanda kwa upande wa wanawake (regional League) ambapo bingwa wa pamoja na mshindi wa pili wanapanda kwenda ligi kuu.

Baada ya miaka mitatu (3) kupita tangu Sasol kudhamini ligi ya wanawake, Banyana Banyana wakafaikiwa kucheza mashindano ya Olympic yaliyofanyika nchini Uingereza mwaka 2012. Pia ABSA kupitia regional league wamechangia kuzalisha wachezaji wengi, zaidi ya timu 144 huwa zinashiriki kupitia kanda 16.

Wakati SAFA waliweza kuishawishi Sasola pamoja na ABSA kuanzisha ligi ya wanawake kupitia mafanikio ya Banyana Banyana, shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF wametangaza ligi ya wanawake kuanza rasmi November 1 mwaka huu huku wakiziacha timu zikiwa kama yatima.

Huko Mwanza moja ya timu imeanza kuchangiwa hadi maji ya kunywa, TFF hawajali kuhusu hili.  Taarifa rasmi kutoka shirikisho ni kwamba hakutokuwa na zawadi kwa bingwa wala wachezaji ambao watafanya vizuri kwenye ligi hiyo.

Vyama vya mikoa vimebebeshwa mzigo wa kuziangalia timu pamoja na kuandaa michezo. Kama hivi vyama vya mikoa ndio zimekuwa chanzo cha malalamiko juu ya upangaji matokeo kwenye ligi daraja la kwanza, je kuwakabidhi ligi vyama vya mikoa sio kutambulisha tena upendeleo na upangaji matokeo?

Sote tunajua kama mpira umekuwa ni ajira, je bila ya wadhamini wachezaji watalipwa vipi pia watasafiri vipi hali ya kuwa vyama vya mikoa vina hali mbaya? Ni ngumu kupata ligi ya ushindani wa kweli kama timu kiuchumi hazipo imara.

Ilikuwa wakati sahihi TFF kutumia mafanikio ya Kilimanjaro Queens ambayo wameyapata kwenye CECAFA ambayo ilifanyika nchini Uganda kama moja ya kishawishi kutafuta wadhamini ambao wangesaidia kupatikana kwa ligi bora ya wanawake.

Kucheza kwa kujitolea tutakuwa bado tunajidanganya, hatutoweza kupata ushindani wa kweli kupitia ligi ya ridhaa.
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget