BAADA ya kusumbuliwa na maumivu ya Mgongo aliyoyapa kwenye mazoezi ya timu ya taifa Taifa Stars kiungo Said Juma amerudishwa nyumbani na kocha Mart Nooij ikiwa ni siku moja baada ya timu hiyo kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Swaziland juzi usiku kwenye michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini.

Kocha ameamua kumrudisha mchezaji huyo anayeichezea klabu ya Yanga, kutokana na tatizo lake kuhitaji muda mrefu wa matibabu.
Msemaji wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Baraka Kizuguto amesema kwamba Said Juma amerudi nyumbani  kwa ajili ya vipimo zaidi na matibabu.