wapiga kura wakiwa katika foleni wakisubiria kupiga kura (picha na charles chami) |
Baaba ya mwaka mmoja na nusu kutokuwa na serekali ya
wanafunzi chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha kimepata
serikali mpya baada ya kufanyika uchaguzi wa kidemokrasia
mapema leo chuoni hapo.
Wanafunzi wa chuo hicho wamejitokeza kwa wingi katika kituo cha kupiga kura na kupata haki yao ya
msingi ya kumchaguwa kiongozi wanaemtaka atakaewaongoza kwa kwa kipindi cha
mwaka mmoja
Mbele ni Bwana Agape msumari akiwa anaitumia haki yake ya msingi ya kupiga kura (picha na charles chami) |
Nafasi ambazo zilikuwa zikwaniwa ni pamoja na nafasi ya
afisa mausiano (P.R.O), Katibu, Makamu wa raisi
na Raisi ambapo katika nafasi ya ukatibu ilikuwa inawaniwa na Inocent
Bambara ambae amepata kura 48, Bogoma wa Bugoma kura 80 na Haji Juma kura 126
kati ya wapiga kura 256 waliojitokeza kupiga kura
Haji Juma katibu wa AJTC (picha na charles chami) |
Nafasi nyingine zilizokuwa
zikiwaniwa ni Afisa mausiano (P.R.O) Wagombea walikuwa wawili ambao ni Benjamin
Jocob alimarufu kama (Big shop beny) aliepata kura 71 na Protte Proffit Mmanga
kura 135
Protte Profit Mmanga P.R.O wa AJTC (picha na charles chami) |
Katika nafasi ya makamu wa raisi ilikuwa na wagombea wane
ambao ni Baraka Charles kura 52, Ruthibetha Fransis kura 77, Robson Jackson
kura 31 na Emma moshi kura 93 na kura zilizo aribika zikiwa ni 3 kati ya wapiga
kura 256
Emma moshi makamu wa raisi katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha (picha na charles chami) |
Nafasi ya mwisho ambayo ilikuwa ikiwaniwa ni nafasi ya
Uraisi ambapo wagombea walikuwa ni wawili waliojitokeza ambao ni Hababi Mohamed
kura 64 na na Kephasi Daniel Ilani ambae
ameibuka kudedea kwa jumla ya kura 191 na kura moja kuaribika kati ya 256
zilizopigwa.
Bwana Kephas Daniel Illani Raisi wa A.J.T.C 2015-216(picha na charles chami) |
JUMLA YA WA WASSHINDI PAMOJA NA KURA ZAO
Jina la mgambea
|
Jumla ya wapiga kura
|
Kura alizopata
|
Kura zilizo aribika
|
Nafasi
|
KEPHASI DANIEL
|
256
|
191
|
1
|
RAISI
|
EMMA MOSHI
|
256
|
93
|
3
|
MAKAMU WA RAISI
|
PROTTE .P.
MMANGA
|
256
|
135
|
HAMNA
|
P.R.O
|
HAJI JUMA
|
256
|
126
|
HAMNA
|
KATIBU
|
Hii inakuwa ni serikali ya nane ya wanafunzi wa chuo hiki
baada kukaa takribani mwaka mmoja na nusu bila serikali, huku ikitanguliwa na
serikali mbili za mwisho ambazo zilikuwa na maswaibu mengi ambazo zilipelekea
kuvunjika kwa serikali hizo
Serikali iliyopita iliyokuwa inaongozwa na raisi George silange ambayo
inasemekana ndo serikali iliyokaa madarakani kwa muda mfupi na kuvunjika
kutokana na serikali yake kutofautiana na uongozi wa juu wa chuo kwenye
mchakato wa kutengeneza katiba ya chuo hicho kitendo ambacho kilimfanya
Silange ajiuzulu kuwa raisi wa A.J.T.C.
George silange raisi wa serikali iliyopita ya AJTC (picha na maktaba) |
Alikadhalika kabla ya serikali hiyo ya silange kulikuwepo na
serikali nyingine iliyovunjika iliyokuwa chini ya David Adriano
Ambapo uongozi wake ulichukuwa uamuzi wa kuandaa tamasha bila idhini ya chuo
kitendo ambacho kilipelekea kuvunjwa kwa serikali yake
David Adriano raisi wa serikali iyovunjika kabla ya George silange (picha na maktaba) |
Serikali hii mpya ya bwana Illani inatabiriwa kuwa serikali
ya amani na inayo fuata ueledi wa uongozi kutokana na aina ya viongozi
waliochaguliwa. Raisi huyo mpya anatarajia kuwasilisha baraza lake la
mawaziri siku ya jumatatu ya tarehe 16 na uongozi wake utakula kiapo siku ya
jumanne.
Post a Comment