http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Timu ya Polisi Dodoma yaamishiwa wilayani Mpwapwa


TIMU ya Soka ya Polisi  Dodoma imekabidhiwa rasmi kwa Wananchi wa Mpwapwa kwa lengo la kuusaidia Mkoa huo uweze kupata timu itakayoshiriki Ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya timu hiyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime amesema wameamua kuwapa timu hiyo wakazi wa Mpwapwa kutokana na kuwa na nia ya dhati ya kuhakikisha Mkoa wa Dodoma unapata timu itakayoshiriki Ligi kuu ya Tanzania Bara.
Kamanda Misime amesema wameamua kuwaachia timu wakazi wa Mpwapwa kutokana na timu hiyo kufanya vibaya katika ligi daraja la kwanza iliyoisha hivi karibuni na timu hiyo kumaliza katika nafasi ya 11 kati ya timu 12 kwa kujikusanyia pointi 19.

“Tumeamua tuanze mapema msimu huu, Tunataka na sisi twende Ligi kuu, Tumeona tutafuta wadau ambao wanaweza aidha kuichukua Timu au kuinunua au tukaiendesha kwa pamoja ili tuweze kufikia hayo malengp ambayo tumejiwekea” Amesema Kamanda Misime.
“Tulipokuwa tunatafuta Wadau, Watu wa Mpwapwa walijitokeza, tukaona wanania ya dhati, wakatupatia mikakati yao tukaona wamejipanga vizuri zaidi na kama tukiwakabidhi timu inaweza ikafika ligi kuu” Amemalizia Kamanda Misime.

Kwa upande wake msemaji wa wadau wa mpwapwa Rashidi Msangi amesema kuwa wameshukuru kupata timu hiyo ambayo wamekuwa wakiiomba kwa muda mrefu zaidi ya miaka miwili iliyopita lakini kwa sasa hatahakikisha tim hiyo inashiriki ligi kuu msimu ujao.


“Tumeanza mazungumzo kwa mwezi mzima leo ndio tumefikia hatma kwamba sasa Mpwapwa tumepewa timu ya Polisi Dodoma ambayo inahamia Mpwapwa, itakuwa ikiitwa Mpwapwa, Wadau baada ya wiki mbili watachagua jina gani ambalo litakuwa linatumika, Tumeongea vizuri kabisa na RPC na tumefikia makubariano mazuri, Na Sio kwamba tumeuziwa timu tumepewa bure” Amesema Rashidi Msangi Msemaji wa Mpwapwa.

Akizungumzia Mipango na mikakati ya kuhakikisha wanafikia malengo Rashidi Msangi nia ni moja tu kupanda ligi kuu.

“Lengo letu mazoezi yanaanza mwisho wa mwezi huu, Tutacheza daraja la kwanza kwa msimu mmoja lengo letu ikiwa ni kwenga Ligi kuu, Tumejiandaa kwa kucheza ligi kuu na sio linguine tena na tutaijenga timu kwa misingi mizuri kbisa sio kubabaisha kama timu nyingine, Kwahiyo nawadhibitishia wanachi wa Mpwapwa kuwa tumepata timu ligi daraja la kwanza ambayo itacheza mwezi wa nane tukiwa na imani itapanda daraja ligi kuu” Amemalizi Kiongozi huyo.
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget