http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

PSG WAIDIWA £180,000 KAMA WATAIFUNGA CHELSEA LEO


Tajiri wa Quatar anaeimiliki timu ya PSG ameaidi wachezaji wa timu yake kama watafanikiwa kuifunga chelsea leo kila mchezaji ataweka kitita cha £180,000 kibindoni PSG wamesafiri mpaka london kutafuta sare ya aina yoyote ya magoli na endapo watatoka sare ya 1-1 basi itaamuliwa kwa mikwaju ya penati.
 

Chelsea wanayo nafasi kubwa ya kusonga mbele baada ya kufanikiwa kupata sare ya 1-1 huko paris ufaranza kwa hiyo leo wanaingia uwanjani wakiwa na faida ya goli moja la ugenini goli lilo wekwa kimiani na beki branslav ivanovic kabla ya mshambuliaji wa kimataifa kutoka uruguay Edson cavan kusawazisha

Itakumbukwa kwamba chelsea na PSG wanakutana kwa mara ya pili mfululizo baada ya chelsea kufanikiwa kuwatowa PSG msimu uliopita katika mashindano hayo baada ya chelsea kupokea kichapo cha goli 3-1 ugenini na katika mchezo wa marudiano msenegali Demba Ba aliwapatia chesea goli la dakika za majeruhi dakika ya 87 ya mchezo 


Mchezo huu unaweza kuwa wa ushindani zaidi kuliko ule ambao chelsea waliwatowa PSG kwani timu ya chelsea imefanya mbadiliko katika kikosi chake kwa kuwaongeza wachezaji kadhaa kama vile Diego Costa, Fabrigas, philipe luiz  pia katika mchezo huo mchezaji kama nemanja matic hakuwepo


Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget