http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

YANGA YAKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WAO DAR BAADA YA KUICHAPA BDF 2-0 TAIFA

mashabiki wa yanga wakionyesha furaha zao baada ya kuifunaga BDF katika dimba la taifa jijini dar
MABAO mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Amissi Tambwe yalitosha kuifanya timu ya Yanga kunza vyema michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF, kwa kuifunga mabao 2-0 BDF XI ya Botswana katika mchezo wa hatua ya awali uliofanyika uwanja wa taifa Dar es Salaam jioni hii.
Ushindi huo unaiweka Yanga katika mazingira mazuri ya kusonga mbele kucheza hatua ya pili endapo itatoka sare au kupata ushindi katika mechi ya marudiano itakayochezwa wiki mbili zijazo Gaborone Botswana.
Katika mchezo huo BDF XI, walionekana kucheza kwa kujihami muda wote wa mchezo na kuwapa nafasi Yanga kuutawala mchezo huo na kulishambulia lango lao na kufanikiwa kupata bao la mapema dakika ya 1 likifungwa kwa kichwa na mchezaji wa zamani wa Amissi Tambwe aliyemalizia mpira wa krosi iliyochongwa na Haruna Niyonzima.
Bao hilo la mapema lilionekana kuwatoa uwanjani BDF XI, na kuwafanya Yanga kuzidi kuliandama lango lao na kutengeneza nafasi nyingi ambazo washambuliaji wake Simon Msuva Mrisho Ngasa na Andrew Coutinho walishindwa kuzitumia na kufanya matokeo kubaki hivyo hadi mapumziko wenyewe wakiwa wamefika kwenye lango la Yanga mara mbili tu.
Tambwe aliifungia Yanga bao la pili katika dakika ya 56 safari hii akiunganisha kwa kichwa krosi iliyochongwa na winga machachari Mrisho Ngasa na kumpoteza a kipa wa BDF XI Takudzwa Ndoro,
Dakika ya 64, 65 na 67 lango la BDF XI lilikuwa katika hekaheka, lakini Nadir Haroub, Andrey Coutinho na Haruna Niyonzima kwa nyakati tofauti walishindwa kutumbukiza mpira wavuni. Mshambuliaji wa BDF XI Vicent Nzombe, nusura aifungie timu yake bao la kufutia machozi baada ya kumlamba chenga Mbuyu Twite lakini akashindwa kumalizia vyema shuti lake likatoka nje ya lango.
Kabelo Seakanyeng naye aliweza kupata nafasi nzuri katika dakika ya 76 kufuatia kuunasa mpira uliokosewa na Haruna Niyonzima lakini shuti alilopiga lilidakwa kiufundi na kipa wa Yanga Ally Mustaph ‘Barthez’
Yanga ambayo ilichezea kwa kubwa zaidi katika kipindi cha pili iliwatoa Andrew Coutinho na Amisi Tambwe na nafasi yao kuchukuliwa na Kpah Sherman na Jeryson Tegete ambao nao waliongeza kasi ya mashambulizi lakini walishindwa kubadili matokeo.
Muda mwingi wachezaji wa BDF XI walionekana walionekana kufanya mashambulizi ya kushtukiza huku wakipoteza muda kwa kujiangusha lakini mwamuzi Thierry Nkurunziza alikua mkali na kumwonyesha kadi ya njano Pelontle Lerole huku kwa upande wa Yanga akiwaonyesha kadi za njano Kelvin Yondani na Ally Mustapha ‘Barthez’.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo kocha wa BDF XI Letang Kgengwenyane ameiambia Goal mchezo ulikuwa mgumu na alifuraishwa na kiwango na nidhamu ya mchezo iliyoonyeshwa na wapinzani wao Yanga ambao waliweza kubaini mbinu zao za kutaka sare na kupata matokeo hayo.
Kocha huyo amesema baada ya kumalizika kwa mchezo huo ameweza kukijua vyema kikosi cha Yanga na wanarudi nyumbani Botswana kwa ajili ya kufanya marekebisha ya mapungufu waliyoyaona na kudhibiti kasi ya Yanga ili dakika 90 za mechi ya marudiano waweze kuzitumia kwa kulipiza kisasi na kusonga mbele hatua inayofuata.
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget