http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

YANGA YAITUNGUWA PRISONS 3-0 COUTINHO AONGOZA MAUWAJI SOKOINE


YANGA SC imeitungua Tanzania Prisons mabao 3-0 katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa CCM Sokoine, Mbeya.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Saimon Msuva (dakika ya 3, 62’ na Andrey Coutinho 11’).
Kwa matokeo hayo, Yanga wameishusha Azam kileleni baada ya kufikisha pointi 28 katika mechi 14 walizocheza na wanawaacha Azam nafasi ya pili wakiwa na pointi 26 kwa mechi 14 walizocheza  baada ya jioni hii kutoka suluhu (0-0) na Ruvu Shootings uwanja wa mabatini, Pwani.
Licha ya kuwazidi Azam kwa pointi, Yanga pia wamewazidi wanalambalamba wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Azam wamefunga magoli 22 na kufungwa 12, tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni 10, wakati Yanga wao wamefunga magoli 18 na kufungwa 7, tofauti ni 11.
Ushindi wa leo ni salamu tosha kwa Mbeya City fc ambao watachuana na Yanga katika uwanja wa Sokoine, jumapili ya wiki hii.
Tanzania Prisons wameendelea kuburuza mkia wakijikusanyia pointi 11 tu katika mechi 14 walizoshuka dimbani.
REPOTI YA MECHI
Mapema dakika ya 3’ Saimon Happygod Msuva aliifungia Yanga bao la kuongoza akimalizia mpira wa kona uliochongwa na kiungo mshambuliaji raia wa Brazil, Andrey Coutinho.
Msuva aliruka juu sambamba na kipa na mpira ulipotua aliugusa kwa mbali na ukamponyoka mlinda mlango na kuzama goli.
Wachezaji wa Prisons walihamaki wakiamini Msuva amemsukuma kipa, lakini mwamuzi akahesabu bao.
Bao la pili lilifungwa dakika ya 11’ ya kipindi cha kwanza ambapo Coutinho alipiga shuti la kawaida, beki wa Prisons akiwa katika harakati za kuokoa alijifunga mwenyewe.
Yanga waliendelea kucheza vizuri, wakigongeana pasi na kufika eneo la hatari la Prisons, lakini safu ya Prisons ilifanya vizuri licha ya kupata misukosuko.
Katika kipindi hicho, Prisons walitulia baada ya kufungwa na kupata nafasi kadhaa, lakini walishindwa kuzitumia.
Mpaka dakika 45’ za kipindi cha kwanza zinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili, Prisons walianza kutafuta mabao ya kuzawazisha, lakini Yanga waliendelea kuonesha uzoefu wao wakiwatuliza vizuri.
Katika dakika ya 62’ Andrey Coutinho aliingiza kona maridadi na Msuva akapiga kichwa ‘ndosi’  na kuzamisha goli la tatu.
Msuva alipata upenyo huo kutokana na uzembe wa beki wa Prisons, Salum Kimenya aliyekuwa anamuangalia tu wakati akimtoka kupiga kichwa.
Coutinho leo hii amefunga goli na kusababisha magoli mawili ya Msuva kutokana na mipira yake ya kona.
Msuva amefikisha mabao 6 msimu huu, magoli mawili nyuma ya kinara wa kupachika mabao, mshambuliaji wa Azam fc, Didier Fortune Kavumbagu.

Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget