Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC wamekubali
kuipisha Yanga kileleni baada ya kabanwa huko mlandizi
Azam FC imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya JKT Ruvu katika
mechi iliyochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi, koani Pwani.
Sare hiyo ya bila mabao, inaifanya Azam FC kufikisha pointi 26
wakati Yanga ambayo imeibuka na ushindi dhidi ya Prisons inafikisha pointi 28.
Azam FC ndiyo iliyokuwa inaongoza kwa kuwa na pointi 25 sawa na Yanga
lakini tofauti ilikuwa ni mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika kipindi cha kwanza dakika 15 za kwanza, Azam FC
ilishambulia zaidi, lakini washambuliaji wake John Bocco na Kipre Tchetche
hawakuwa makini.
Kipindi cha pili, mambo yalibadilika na JKT kutawala huku
wakionekana kuwasumbua Azam FC, hata hivyo nao hawakuwa makini kumalizia nafasi
walizozipata.
Mhezo huo uliokuwa wa
kiporo ndio wa mwisho wa kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara.
Post a Comment