Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans, kesho wanatarajia kukwea pipa na kuelekea Nchini Botswana , kuminyana na BDF XI katika mchezo wa marudiano kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za makao makuu ya klabu hiyo, Mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, amesema kuwa Jumala ya wachezaji 20 ndio watakao ondoka hiyo kesho kupambana na wanajeshi hao wa Botswana.
Katika safari hiyo Yanga watamkosa Kiungo wao mshambuliaji ambaye kwasasa ameonyesha kulielewa vyema soka la Bongo, Andrey Coutinho, raia wa Brazil, baada ya kuwa mgonjwa kitu ambacho kinafanya Yanga waweze kumuacha Dar es salaam hiyo kesho.
Kocha mkuu wa Wanajangwani hao Hans Van De Pluijm, amesema kuwa Coutinho aliumua katika mchezo wa juzi dhidi ya Mbeya city kwenye mechi ya ligi ambapo Yanga iliibuka na Ushindi wa mabao 3-1.
Nyota wa Yanga ambao kesho wanakwea pipa ni Makipa, Deogratius Munishi ‘Dida’ Ally Mustafa ‘Barthez’, Mabeki, Mbuyu Twite, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani.
Wengine ni Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Salum Tellela, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngassa ‘ Uncle’, Simon Msuva, Amisi Tambwe, Kpah Sherman pamoja na Mchezaji wa zamani wa Polisi Morogoro, Dany Mrwanda.
Post a Comment