Cameroon sasa wameenda Brazil baada ya mzozo kuhusu marupurupu yao kutatuliwa.
Wachezaji hao , almaarufu 'Indomitable Lions' walikuwa wamesusia kuingia ndegeni hadi marupurupu yao yaongezwe.Wachezaji hao walikuwa wakilalamikia kiwango cha fedha £61,000 ambazo walikuwa wamepangiwa kupewa wakisema hazingetosha.
Haijabainika vyema ni idadi gani walichoongezewa ndio wakakubali safari.
Hata hivyo rais wa shirikisho la soka la Cameroon Bw.Joseph Owona amesema 'baada ya kuweka kila kitu wazi ,mzozo huo umetatuliwa na sasa hamna tatizo'.
Tatizo lililopo sasa kwa masimba hao ni kupata mkakati madhubuti wa kukabiliana vilivyo na timu za kundi lao A ambamo wamo miamba ya soka wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.www.skychami.com
Post a Comment