NANI KIDEDEA DABI ya MERSEYSIDE ambayo itakuwa Dabi ya 221?
Hili ni swali gumu sana kulijibu.
Kwa Misimu miwili iliyopita, Everton wamekuwa wakimaliza Ligi Kuu
England wakiwa juu ya wapinzani wao wa Jadi, Liverpool, lakini katika Mechi 4
walizocheza Everton hawakuifunga Liverpool hata Mechi moja kwa kutoka Sare 2 na
Kufungwa 2.
Msimu huu, Liverpool wameanza kwa moto, wako Nafasi ya Pili,
wameshinda Mechi 7 na wako Pointi 3 mbele ya Everton walio Nafasi ya 6 na
wameshinda Mechi 5.
Hali hii ya Liverpool imesaidiwa sana na ushirikiano wa Mastraika
wao Luis Suarez na Daniel Sturridge ambao kati yao wamefunga Jumla ya Mabao 21.
Everton, Msimu huu, hawajafungwa kwao Goodison Park na ngome yao
ni ngumu kufungika wakiwa wametoka Mechi 6 kati ya 11 za Ligi bila kupigwa hata
Bao moja.
-Emirates Stadium [Jumamosi Saa 12 Jioni]
Hii ni Mechi ambayo, hadi sasa Difensi ngumu kwenye Ligi,
inakutana na Arsenal ambayo imepiga Bao katika Mechi 15 za Ligi mfululizo hadi
Mabingwa Manchester United walipoichapa Arsenal Bao 1-0 katika Mechi yao ya
mwisho ya Ligi Kuu England.
Msimu huu, Southampton wamefungwa Bao 5 tu lakini wanarudi Uwanja
wa Emirates ambao Msimu uliopita walitwangwa Bao 6-1.
Safari hii, Arsenal wataimarika kwa kurudi dimbani kutoka Majeruhi
kulomweka Miezi miwili nje Mchezaji wa zamani wa Southampton, Theo Walcott,
kama ilivyothibitishwa na Meneja Arsene Wenger.
FULHAM v SWANSEA
-Craven Cottage [Jumamosi
Saa 12 Jioni]
Hii ni ‘lala salama’ kwa Meneja wa Fulham, Martin Jol, ambae
anajua fika amekalia kuti kavubaada kupigwa Mechi 3 mfululizo za Ligi na tayari
Klabu hiyo imechukua hatua kudhibiti hali yao mbaya kwa kumwajiri Kocha Mkuu wa
zamani wa Man United Rene Meulensteen ambae Wadau wanahisi huyu ndio atakuwa
‘Meneja mpya!’
HULL v CRYSTAL PALACE
-KC Stadium [Jumamosi Saa
12 Jioni]
Mara ya mwisho kwa Hull City kuifunga Crystal Palace kwenye KC
Stadium ilikuwa Mwaka 2008 wakati Timu zote zilipokuwa Daraja la Championship
na tangu wakati huo Crystal Palace imeshinda mara 2 na Sare 4.
Lakini Hull City, Msimu huu, hawajafungwa kwao wakati Palace
walichapwa Mechi 7 mfululizo hadi Mechi yao ya mwisho walipotoka Sare na
Everton.
NEWCASTLE v NORWICH
-St James’ Park [Jumamosi
Saa 12 Jioni]
Ni miaka 25 imepita tangu Norwich City waifunge Newcastle Uwanja
wa St James’ Park lakini Norwich hii inavujisha Magoli kwani washapigwa Bao 21
kitu ambacho Meneja wao Chris Hughton itabidi akitilie mkazo sana.
Msimu huu, Newcastle, chini ya Alan Pardew, wamefungwa mara moja
tu wakiwa Uwanja wao na wanatinga Mechi hii wakiwa wameshinda Mechi mbili za
Ligi mfululizo.
STOKE v SUNDERLAND
Britannia Stadium [Jumamosi
Saa 12 Jioni]
Ni Mechi inayokutanisha Timu ambazo zinasuasua huku Stoke City
wakiwa hawajashinda Uwanjani kwao tangu Mechi yao ya pili ya Ligi Msimu huu na
Sunderland wakiwa hawajashinda Ugenini kwenye Ligi tangu Mwezi Aprili.
Lakini hivi sasa Timu hizi zinaingia kwenye mabadiliko kwani Stoke
City, chini ya Meneja Mark Hughes, imetoka Sare Mechi mbili mfululizo na
Sunderland, chini ya Gus Poyet, iliifunga Man City katika Mechi yao ya mwisho.
WEST HAM v CHELSEA
-Upton Park [Jumamosi Saa 2
na Nusu Usiku]
Mwaka mmoja uliopita, Carlton Cole alifunga Bao ambalo
liliiwezesha West Ham kuichapa Chelsea Bao 3-1 ukiwa ni ushindi wao wa kwanza
dhidi ya Chelsea tangu Mwaka 2003.
Baada ya hapo Cole aliihama Klabu hiyo lakini sasa amerudi tena na
Chelsea nao wamemrudisha Kocha wao wa zamani Jose Mourinho ambae bado anasuasua
kwenye Ligi na katika Mechi yao ya mwisho walitoka Sare 2-2 huko Stamford
Bridge na West Brom na kunusurika kwa Penati ya utata.
MANCHESTER CITY v TOTTENHAM
-Etihad Stadium [Jumapili
Saa 10 na Nusu Jioni]
Timu zote hizi zinatinga kwenye Mechi hii wakitokea kwenye vipigo
vya kutia uchungu baada City kufungwa na Sunderland Bao 1-0 na Tottenham
kutunguliwa pia 1-0 na Newcastle.
City hawajafungwa kwao Msimu huu lakini Spurs wameshashinda Mechi
3 Ugenini Msimu huu.
CARDIFF CITY v MANCHESTER
UNITED
Cardiff City Stadium
[Jumapili Saa 1 Usiku]
Man
United wanategemea Nyota wao Robin van Persie, ambae ndie alifunga Bao la
ushindi walipoichapa Arsenal Bao 1-0 katika Mechi yao ya mwisho ya Ligi,
atakuwa fiti baada kushindwa kuiwakilisha Nchi yake Netherlands kwenye Mechi za
Kimataifa kutokana na maumivu ya kidole cha Mguuni pamoja na Nyonga.
Lakini Man United itawakosa Michael Carrick na Phil Jones ambao
wameumia na hivyo kulazimika kuwachezesha kwenye Kiungo Anderson, Tom Cleverley
na Ryan Giggs huko Wales ambako hawajakutana na Cardiff City tangu Mwaka 1974
walipoifunga Bao 1-0.
Tegemeo kubwa la Cardiff kwa Magoli ni Kijana wa zamani wa Man
United, Fraizer Campbell, ambae hajafunga kwenye Ligi tangu Mwezi Agosti ambapo
Bao zake 2 ziliiua Man City.
WEST BROM v ASTON VILLA
The Hawthorns [Jumatatu Saa
5 Usiku]
Mara ya mwisho Timu hizi kukutana na Mshindi kupatikana ni Oktoba
2011 wakati West Brom ilipoifunga Aston Villa Bao 2-1 Uwanjani Villa Park.
Lakini tangu hapo, Dakika 270 za Soka zimepita bila mbabe
kupatikana na wakati huu Timu zote zinafanya vyema kwenye Ligi huku WBA ikiwa
imetoka kwenye Mechi iliyozua utata baada ya nusura kuichapa Chelsea Bao 2-1
Uwanjani Stamford Bridge kama si Penati ya utata ya Dakika ya mwisho ya 94
kuipa Chelsea Bao la kusawazisha.
Post a Comment