http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

BARCA,ATLETICO ZAFUZU, WAUNGANA NA BAYERN NA CITY! ETO'O NEA APIGA MBILI ANGALIA MATOKEO YOTE HAPA



WAKATI USIKU HUU Klabu za England, Chelsea na Arsenal, zikishikilia usukani wa Makundi yao ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Klabu za Spain, FC Barcelona na Atletico Madrid, zimefuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 huku zikiwa na Mechi mbili mkononi.
Timu nyingine zilizofuzu Jumanne Usiku ni Mabingwa Watetezi Bayern Munich na Manchester City.
Kila Timu imebakisha Mechi mbili za Makundi ambazo zitachezwa Novemba 26 na 27 na kumalizia Desemba 10 na 11.
CHELSEA 3 SCHALKE 0

 
Bao za Samuel Eto'o Dakika ya 31 na 54, na la Demba Ba Dakika ya 83, Usiku huu zimewapa Chelsea ushindi wa Bao 3-0 kwao Stamford Bridge kwa kuinyuka Klabu ya Germany Schalke na kukamata uongozo wa Kundi E.
Chelsea wakiifunga FC Basel Mechi ijayo huko Uswisi watafuzu.


BARCELONA 3 AC MILAN 1

Wakiwa kwao Nou Camp, Barcelona wameichapa AC Milan Bao 3-1 kwa Bao za Lionel Messi, Penati ya Dakika ya 30 na jingine Dakika ya 83, pamoja na Busquets kwenye Dakika ya 39.
AC Milan walipata Bao lao, ambalo lilifanya Gemu iwe 1-1 wakati huo, kwa juhudu ya Kaka iliyosababisha Beki Pique kujifunga.
 BORUSSIA DORTMUND v ARSENAL

Bao la Dakika ya 62 la Aaron Ramsey kwa kichwa katika shambulio la kwanza la Arsenal limewapa ushindi wa Bao 1-0 huko Signal Iduna Park walipocheza na Borussia Dortmund.
Hii ni Mechi ambayo Dortmund watajilaumu sana kwa kuipoteza kwa jinsi walivyokosa Bao baada ya Bao
FC Basel 1 FC Steaua Bucureşti 1
Chelsea FC 3 FC Schalke 0
Borussia Dortmund 0 Arsenal 1
SSC Napoli 3 Olympique de Marseille 2
Football Club Zenit 1 FC Porto 1 
Club Atlético de Madrid 4 FK Austria Wien 0
AFC Ajax 1 Celtic 0
FC Barcelona 3 AC Milan 1

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget