http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

REAL WALIA NA REFA!!

NEYMAR_IN_BARCA


MAOFISA na WACHEZAJI wa Real Madrid wamenyoosha kidole kwa Refa Alberto Undiano Mallenco baada kuchapwa Bao 2-1 huko Nou Camp hapo Jana katika El Clasico ya kwanza Msimu huu ambayo ilikuwa Mechi ya La Liga.
Bao toka kwa Neymar na Alexis Sánchez ziliipa Timu ya Kocha Gerardo Martino ushindi wa Bao 2-1 huku Bao la Real likifungwa na Jese lakini Real Madrid wamelalamikia kunyimwa Penati mbili.
Dakika chache kabla Haftaimu, Refa Mallenco alipeta Penati baada ya Mpira kumparaza Adriano mkononi wakati akiwa kwenye Boksi la Barca na Penati nyingine
wanayodai Real ni pale Cristiano Ronaldo aliposukumwa na Javier Mascherano ndani ya Boksi.
    Akiongea na Canal Plus, Beki wa Real, Sergio Ramos, alisema: “Kuna vitu huwezi kupigana navyo. Kulikuwa na Penati ya wazi Kipindi cha Kwanza ya kuunawa Mpira na Kipindi cha Pili tukio la Ronaldo. Lakini nadhani Mashabiki wote wa Real watasikia fahari kwa jinsi tulivyopigana hadi Dakika ya mwisho. Ni muda mrefu tangu Barca waonekane wameelemewa na kuamua kupoteza muda ili waokoke!”
Katika La Liga Msimu huu, Barca wameshinda Mechi 9 na wana Pointi 28, wakiwa kileleni Pointi 6 mbele ya Real ambao wako Nafasi ya 3.
Atletico Madrid, wenye Mechi moja mkononi, wako Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 24.
  Nae Mbrazil Neymar, akicheza El Clasico yake ya kwanza kabisa, amesema: “Nimefurahi sana kufunga Bao spesho lakini nimefurahi zaidi kupata Pointi 3! Ilinifurahisha sana kufunga katika Mechi ambayo kila Mchezaji anataka kushiriki. Sidhani ushindi huu ndio umeamua hatima ya Ubingwa. Bado tuko mbali na Ubingwa haujaisha

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget